Sepah yaua magaidi wa kundi linalopinga Mapinduzi ya Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i9952-sepah_yaua_magaidi_wa_kundi_linalopinga_mapinduzi_ya_kiislamu
Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) limetangaza kuwa limeangamiza magaidi kadhaa wa kundi wa wapinzani wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mapigano yaliyotokea katika eneo la kaskazini magharibi mwa Iran.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 25, 2016 15:15 UTC
  • Sepah yaua magaidi wa kundi linalopinga Mapinduzi ya Kiislamu

Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) limetangaza kuwa limeangamiza magaidi kadhaa wa kundi wa wapinzani wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mapigano yaliyotokea katika eneo la kaskazini magharibi mwa Iran.

Taarifa iliyotolewa na kambi ya Hamza Sayyidu Shuhadaa ya kikosi cha Jeshi la wa Mapinduzi ya Kiislamu imesema mapigano hayo yalitokea katika eneo la mpakani la Mahabad katika mkoa wa Azerbaijan Magharibi na kwamba magaidi kadhaa wameuawa katika mapigano hayo.

Taarifa hiyo imesema operesheni ya kuwasaka na kuwaangamiza magaidi wengine ingali inaendelea.

Siku chache zilizopita Waziri wa Usalama Iran, Mahmoud Alavi alitangaza kuwa wizara hiyo imewakamata magaidi kadhaa waliokuwa wamepanga kutekeleza mashambulizi katika maeneo 50 nchini Iran.

Wanachama wa kundi hilo la kigaidi wamekiri kwamba walifadhiliwa na Saudi Arabia na Marekani.