Hongera katika siku kuu ya Ghadir Khum
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i99614-hongera_katika_siku_kuu_ya_ghadir_khum
Leo Ijumaa mwaka 1444 Hijria Qamaria sawa na 7 Julai 2023 inasadifiana na siku kuu ya Ghadir Khum ambayo ni idi kubwa ya Waislamu.
(last modified 2026-07-03T11:45:53+00:00 )
Jul 06, 2023 23:40 UTC
  • Hongera katika siku kuu ya Ghadir Khum

Leo Ijumaa mwaka 1444 Hijria Qamaria sawa na 7 Julai 2023 inasadifiana na siku kuu ya Ghadir Khum ambayo ni idi kubwa ya Waislamu.

Katika sikku kama ya leo miaka 1444 iliyopita Mtume Muhammad (SAW) akiwa katika safari yake ya mwisho ya Hija, kwa amri ya Mwenyezi Mungu alimtangaza Imam Ali bin Abi Twalib AS kuwa kiongozi wa Waislamu wote baada yake. 

Siku hiyo Mtume SAW alitoa hotuba mbele ya hadhara kubwa ya Waislamu kisha akashika mkono wa Ali bin Abi Twalib na kusema: "Kila mtu ambaye mimi ni kiongozi wake basi huyu Ali pia ni kiongozi wake. Mwenyezi Mungu ampende atakayempenda, na amfanyie uadui atakayemfanyia uadui." Mtume SAW pia aliwausia Waislamu kushikamana na Qur'ani na Ahlubaiti wake na akasema viwili hivyo havitatengana hadi vitakapomkuta yeye katika Hodhi ya Kauthar, Siku ya Kiyama. 

Idd Ghadir Khum, pia inafasiriwa kama Idd al-Akbar (Iddi kubwa zaidi) katika umma wa Kiislamu . Iddi hii inaashiria kukamilika juhudi za Mitume wote wa Mwenyezi Mungu.

Waumini  katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika siku hii huenda kutembelea Sadat au Masharifu yaani watu ambao nasaba yao inafungamana na ile ya Mtume Muhammad SAW. Aidha katika siku hii waumini huhudhuria sherehe mbalimbali pamoja na kusikiliza hotuba na mawaidha.

Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran linawapongeza Waislamu kote duniani na wapenda uhuru popote pale walipo kwa mnasaba wa kuwadia siku kuu ya  Eid Ghadir Khum.