Marekani yakiri kwamba Iran haina nia ya kuzalisha silaha za nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i99792-marekani_yakiri_kwamba_iran_haina_nia_ya_kuzalisha_silaha_za_nyuklia
Licha ya madai ya huko nyuma ya maafisa wa nchi za Magharibi na Wazayuni, taasisi ya ujasusi ya Marekani imekiri kwamba Iran haifuatilii silaha za nyuklia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 11, 2023 10:53 UTC
  • Marekani yakiri kwamba Iran haina nia ya kuzalisha silaha za nyuklia

Licha ya madai ya huko nyuma ya maafisa wa nchi za Magharibi na Wazayuni, taasisi ya ujasusi ya Marekani imekiri kwamba Iran haifuatilii silaha za nyuklia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, tathmini ya kijasusi iliyofanywa na Marekani imebainisha kuwa Iran haina nia ya kumiliki silaha za nyuklia.

Kukiri huko kumetangazwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Ujasusi wa Taifa wa Marekani (ODNI), wakati maafisa wa nchi za Magharibi na utawala wa Kizayuni wa Israel wakiwa bado wanafanya jitihada za kuendeleza mradi wao ulioshindwa wa kuenenza propaganda chafu dhidi ya Iran.

Iran daima imekuwa ikitangaza kwamba, haina mpango wa kuzalisha bomu la nyuklia, na kwamba bomu la nyuklia halina nafasi yoyote katika itikadi ya Kiislamu ya Iran.

Hatua ya taasisi hiyo ya masuala ya ujasusi ya Marekani inafuatia ile ya mkuu wa zamani wa kitengo cha CIA kuhusu Iran, Norman Roule, aliyewahi kukiri kwamba Iran haina nia ya kutengeneza silaha za nyuklia.

Vilevile, Jumuiya ya Ujasusi ya Marekani (United States Intelligence Community) ilikiri katika ripoti yake ya kila mwaka ya tarehe 8 Machi kwamba Tehran kwa sasa haifanyi shughuli zozote za utengenezaji wa silaha za nyuklia.