Kongamano la Imam Hussein AS lafanyika Kampala, mji mkuu wa Uganda
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i99936-kongamano_la_imam_hussein_as_lafanyika_kampala_mji_mkuu_wa_uganda
Kongamano la Imam Hussein (AS) limefanyika katika eneo la Afrika Mashariki katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 15, 2023 04:16 UTC
  • Kongamano la Imam Hussein AS lafanyika Kampala, mji mkuu wa Uganda

Kongamano la Imam Hussein (AS) limefanyika katika eneo la Afrika Mashariki katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, sambamba na kukaribia mwezi wa Mfunguo Nne wa Muharram na kutokana na umuhimu wa kuyatambulisha mapambano na mwamko wa Ashura na Njia ya Fikra ya Imamu Hussein AS, kongamano la Imam Hussein limefanyika jijini Kampala kwa kuhudhuriwa na mashekhe na wanazuoni wa Kiislamu pamoja na shakhsia wengine wa kidini na kisiasa kutoka Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda na Burundi.
 
Washiriki wa Kongamano la Imam Hussein AS jijini Kampala, Uganda

Itakumbukwa kuwa wakati Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alipokuwa ziarani nchini Uganda alishiriki katika kongamano la Imam Hussein (AS) na kutoa hotuba kwa washiriki na wafuasi wa Ahlul Bayt  AS kuhusu mapambano na mwamko wa Ashura.

 
Hafla za maombolezo ya Imam Hussein (AS) zinafanyika pia katika baadhi ya nchi za Kiafrika na kuhudhuriwa kwa wingi na wafuasi na wapenzi wa Ahlul-Bayt AS, watu wa Nyumba Tukufu ya Bwana Mtume Muhammad SAW.../