-
Rais wa Iran: Tunataraji vita na mauaji ya kimbari yatamalizika katika mwaka mpya
Dec 31, 2024 04:13Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameelezea matumaini yake kuwa dhulma, machafuko, vita na mauaji ya kimbari yatakoma katika mwaka mpya wa 2025.
-
Pezeshkian: Hatua za kivitendo za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuimarisha amani na usalama katika eneo
Dec 30, 2024 09:11Rais Masoud Pezeshkian ameeleza kuwa mtazamo na hatua za kivitendo za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni za kueneza amani na kudumisha usalama katika ukanda huu na baina ya nchi zote za Kiislamu; na ametaka kuwepo ushirikiano mkubwa zaidi kati ya Iran na Oman katika uwanja huo.
-
Araghchi asisitiza kuundwa serikali jumuishi nchini Syria
Dec 30, 2024 09:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitizia wajibu wa kuundwa serikali jumuishi nchini Syria. Sayyid Abbas Araqchi ameeleza haya leo katika kikao na waandishi wa habari hapa Tehran akiwa na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Sayyid Badr Albusaidi.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akutana na wenzake wa UAE na Oman
Dec 30, 2024 04:24Waziri wa Mambo wa Iran Abbas Araghchi na mwenzake wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan wamezungumzia uhusiano wa nchi mbili na matukio ya hivi karibuni katika eneo hilo.
-
Mcheza chess wa Iran akataa kushindana na mpinzani wa Israel akiwaunga mkono Wapalestina
Dec 30, 2024 00:15Katika kuwaunga mkono watu wa Palestina, mchezaji wa chess wa Iran amekataa kushindana na mwakilishi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mashindano ya World Rapid Chess Championship 2024 huko New York.
-
Jeshi la IRGC lasema liko tayari kulinda usalama wa Iran
Dec 29, 2024 09:41Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limeeleza utayari wake kamili wa kulinda usalama wa Iran na kukabiliana na njama za adui anayelenga kuleta machafuko na uchochezi nchini.
-
Makubaliano ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na China ya kutekeleza mpango wa kistratejia wa nchi mbili
Dec 29, 2024 08:38Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na China wametathimini kuwa chanya mchakato unaopiga hatua wa kutekeleza vipengee vya ushirikiano wa kistratejia katika miaka ya karibuni.
-
Araghchi: Mkataba wa ushirikiano wa miaka 25 ni msingi thabiti wa kuendeleza uhusiano Iran na China
Dec 29, 2024 04:14Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhurii ya Kiislamu ya Iran ameashiria historia ndefu na imara ya uhusiano kati ya mataifa mawili ya Iran na China, na kueleza kuwa, Tehran haitaacha juhudi zozote za kutumia fursa nyingi na Beijing, na kwamba, mpango wa miaka 25 ni msingi thabiti wa kupanua ushirikiano katika nyanja mbalimbali.
-
Iran: Marekani inalenga kuwapora Waislamu, haitafanikiwa chochote nchini Syria
Dec 28, 2024 23:23Jeshi la Iran linasema kutimuliwa kwa Rais Bashar al-Assad wa Syria na wanamgambo wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni ni njama ya Wamarekani na Wazayuni, lakini Marekani haitafanikiwa lolote katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Iran: Shambulio la Israeli katika Hospitali ya Kamal Adwan ni 'uhalifu mbaya wa kivita'
Dec 28, 2024 23:23Iran imekemea shambulio la kikatili la utawala wa Israel kwenye Hospitali ya Kamal Adwan katika eneo la kaskazini mwa Gaza kama “uhalifu mbaya wa kivita” na sehemu ya mauaji ya kimbari yanayoendelea kwenye ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu na kusema kimya cha taasisi muhimu za kimataifa kuhusu suala hilo kama “hakikubaliki.”