-
Balozi wa Iran nchini Russia na Mufti wa Moscow wasisitiza ushirikiano wa kidini
Dec 27, 2025 08:47Kazem Jalali, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Russia amekutana na kufanya mazungumzo na Albir Hazrat Krganov, Mufti wa Moscow na Mwenyekiti wa Baraza la Kiroho la Waislamu wa Russia, na kujadili namna ya kupanua ushirikiano wa kidini.
-
Hamas: Kutambuana kati ya "Israel" na "Somaliland" ni mfano hatari
Dec 27, 2025 08:41Harakati ya Kiislamu ya kupigania ukombozi wa Palestina (Hamas) imetangaza leo Jumamosi upinzani wake dhidi ya tangazo la utawala uliojitenga na Somalia katika eneo la "Somaliland" la kutambuana rasmi na Tel Aviv, ikisisitiza kuwa hatua hiyo "ni mfano hatari na jaribio lililoshindwa la kupata uhalali bandia dola vamizi linalohusika katika uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari."
-
Ujumbe wa kwanza wa Umoja wa Mataifa wawasili El Fasher kutathmini hali ya mambo
Dec 27, 2025 07:46Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema shirika hilo limefanikiwa kupeleka ujumbe wa tathmini huko El Fasher, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan.
-
Ujumbe Kiongozi Muadhamu kwa Umoja wa Jumuiya za Wanafunzi wa Kiislamu barani Ulaya; kubebwa na Iran bendera ya kukabiliana na utaratibu usio wa kiadilifu
Dec 27, 2025 07:41Katika ujumbe wake kwa mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Jumuiya za Wanafunzi wa Kiislamu barani Ulaya, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Taifa la Iran kwa kutumia uwezo wake linaweza kusimama na kutoa wito wa thamani za Kiislamu kwa walimwengu kwa sauti kubwa kuliko wakati mwingine wowote."
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Marekani inatumia 'sheria ya mwituni' badala ya diplomasia
Dec 27, 2025 06:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, amesema kwamba Marekani inafuata "sheria ya mwituni" badalaya ya diplomasia, ikitumia nguvu na vikwazo ili kuendeleza maslahi yake.
-
Ayatullah Khamenei: Mashambulizi ya Marekani na Israel yalishindwa kwa hima na ushujaa wa vijana wa Iran
Dec 27, 2025 06:18Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesema mashambulio makubwa ya jeshi la Marekani na mwanaharamu wake katika eneo la Magharibi mwa Asia yalishindwa kutokana na ubunifu, ushujaa na kujitolea kwa vijana wa Iran ya Kiislamu.
-
Muungano wa waandishi wa habari wa Palestina: Israel 'inawanyamazisha' waandishi habari kwa mashambulizi ya kimfumo
Dec 27, 2025 06:17Chama cha Waandishi wa Habari cha Palestina kimeulaani utawala wa Israel kwa kufuata sera ya kimfumo ya kuwalenga waandishi wa habari, kikisema ukatili unaofanywa dhidi ya vyombo vya habari umeongezeka sana mwaka 2025 kama sehemu ya njama za kuzuia ripoti za Wapalestina.
-
Umoja wa Mataifa waisihi Guinea kukomesha ukiukwaji wa haki kabla ya uchaguzi
Dec 27, 2025 03:11Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ameitaka serikali ya Guinea kukomesha mara moja vitendo vya vitisho na ukiukwaji wa haki za binadamu kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika kesho Jumapili tarehe 28 Desemba, akionya kuwa hali ya sasa inahatarisha uhalali wa mchakato wa uchaguzi.
-
Israel yalaaniwa vikali kwa kutambua Somaliland kama nchi huru
Dec 27, 2025 03:11Utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza kutambua eneo la 'Somaliland, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili.
-
Wataalamu: Operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Nigeria inalenga kugawa taifa
Dec 27, 2025 03:10Wataalamu wametilia shaka lengo la Rais wa Marekani, Donald Trump, katika mashambulizi ya kijeshi nchini Nigeria kwa kisingizio cha kupambana na magaidi wa kundi la DAESH (ISIS/ISIL) kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.