Mbunge wa Marekani asema Trump ni mtendajinai
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138114-mbunge_wa_marekani_asema_trump_ni_mtendajinai
Mbunge wa chama cha Democratic wa Marekani amemtaja Donald Trump Rais wa nchi hiyo kuwa ni mhalifu mtendajinai.
(last modified 2026-05-02T10:02:51+00:00 )
May 02, 2026 10:01 UTC
  •  Ilhan Omar
    Ilhan Omar

Mbunge wa chama cha Democratic wa Marekani amemtaja Donald Trump Rais wa nchi hiyo kuwa ni mhalifu mtendajinai.

Katika ujumbe wake uliotumwa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Ijumaa baada ya kusambaa video ya matamshi ya Donald Trump huko Florida, Ilhan Omar aliandika: "Huu ni upuuzi wa kichaa kutoka kwa mhalifu mwenye rekodi ya makosa 34 ya jinai, ameshtakiwa kwa ubakaji na anatuhumiwa kunyanyasa watoto."

Katika hotuba yake huko Florida, Trump alirudia uvumi dhidi ya Ilhan Omar, mwakilishi Mwislamu na Mmarekani mwenye asili ya Somalia kutoka Minnesota, ambao ulipingwa muda mrefu uliopita. Rais wa Marekani alidai katika taarifa kali kwamba: "Ninaamini alioana na kaka yake, jambo ambalo ni kinyume kabisa na sheria."

Ilhan Omar pia ameeleza kuwa: Jina la Donald Trump limekaririwa mara 38,000 katika kesi ya mhalifu wa ngono na ubakaji dhidi ya watoto, Jeffrey Epstein.

Katika jumbe wake wa hapo awali, mwakilishi huyo wa Bunge la Marekani, aliashiria nafasi kubwa ya rais wa nchi hiyo katika kesi ya Epstein na kutangaza kwamba Trump ni kiongozi wa kundi linalounga mkono wanyanyasaji wa watoto kingono.

Kesi kubwa ya ufuska na ufisadi ya Jeffrey Epstein, mfanyabiashara Myahudi, mhalifu wa ngono na mtakasaji pesa, imeweka kivuli kizito kwenye anga ya umma ya siasa za Marekani kwa miaka mingi sasa.