-
Umoja wa Mataifa waisihi Guinea kukomesha ukiukwaji wa haki kabla ya uchaguzi
Dec 27, 2025 03:11Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ameitaka serikali ya Guinea kukomesha mara moja vitendo vya vitisho na ukiukwaji wa haki za binadamu kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika kesho Jumapili tarehe 28 Desemba, akionya kuwa hali ya sasa inahatarisha uhalali wa mchakato wa uchaguzi.
-
Israel yalaaniwa vikali kwa kutambua Somaliland kama nchi huru
Dec 27, 2025 03:11Utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza kutambua eneo la 'Somaliland, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili.
-
Wataalamu: Operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Nigeria inalenga kugawa taifa
Dec 27, 2025 03:10Wataalamu wametilia shaka lengo la Rais wa Marekani, Donald Trump, katika mashambulizi ya kijeshi nchini Nigeria kwa kisingizio cha kupambana na magaidi wa kundi la DAESH (ISIS/ISIL) kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
-
Waziri Mkuu wa Sudan akataa vikosi vya kimataifa, akubali uangalizi wa masharti
Dec 27, 2025 03:09Waziri Mkuu wa Sudan, Kamil Idris, alisema Ijumaa kwamba serikali ya nchi hiyo haitakubali kupelekwa kwa vikosi vya kimataifa katika mchakato wowote wa amani ujao, ingawa imekubali uwepo wa uangalizi kwa masharti.
-
Yemen yasema iko tayari kwa vita, yawataka Waislamu wawe macho
Dec 27, 2025 03:08Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen amesema taifa hilo linaendelea kujiandaa usiku na mchana kwa duru ijayo ya vita visivyoweza kuepukika dhidi ya Marekani na Israel, akiahidi kuwa harakati za Muqawama au mapambano ya Kiislamu za Kiyemeni hazitasimamishwa wala kupokonywa silaha.
-
Taasisi za Palestina: Maelfu ya wafungwa wanateswa katika magereza ya Israel
Dec 27, 2025 02:31Asasi mbili za Kipalestina yametangaza kwamba, zaidi ya mateka na wafungwa 9,300 wa Palestina wanaoshikiliwa katika magereza na vituo vya kuzuiliwa vya Israel wanakabiliwa na "mateso yaliyopangwa."
-
Iran yalaani vikali shambulio baya la kigaidi nchini Syria
Dec 26, 2025 23:17Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali shambulio la kigaidi dhidi ya Waislamu katika Msikiti wa Imam Ali ibn Abi Talib (AS) katika Mkoa wa Homs nchini Syria ambalo limeua shahidi na kujeruhi watu wengi wakati wa Sala ya Ijumaa ya jana Msikitini humo.
-
Serikali ya Ethiopia yashtakiwa kwa kuwatelekeza wakimbizi
Dec 26, 2025 23:16Shirika la Kutetea Haki za Binadamu nchini Ethiopia, la Human Rights First limeishtaki serikali ya Ethiopiia kwa kile lilichodai hatua ya serikali ya Addis Ababa ya kuwatelekeza wakimbizi.
-
Umoja wa Mataifa: Kujengwa vitongoji vipya Ukanda wa Gaza ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa
Dec 26, 2025 23:06Ripota maalum wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kukuza nidhamu ya kidemokrasia na uadilifu kimataifa amesema kuwa, kauli za Waziri wa Vita wa Israel kuhusu kuanzishwa kwa vitongoji vipya katika Ukanda wa Gaza ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
-
Mji wa Shiraz; moja ya vituo vikuu vya utalii wa kimatibabu Asia Magharibi
Dec 26, 2025 22:56Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Shiraz katika Mkoa wa Fars, Iran, kimechukua hatua kubwa za kubadilisha jiji hili kuwa kitovu cha utalii wa matibabu katika Asia Magharibi kwa kufikia makubaliano ya ushirikiano na Uzbekistan na kupanga kupanua mazungumzo na nchi zingine jirani.