-
Lavrov: Nchi za Magharibi zinachochea migawanyiko Afrika
Oct 15, 2025 08:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov amesema kivuli cha ukoloni kinasalia kuwa chanzo kikuu cha migogoro barani Afrika, na wakoloni wa zamani, sasa hivi wanajaribu kukwepa uwajibikaji kwa kuilaumu Moscow.
-
Jihadul Islami: Muqawama haujaafiki kipengee cha kuweka chini silaha
Oct 15, 2025 07:50Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Jihadul Islami ya Palestina amepuuzilia mbali wazo la kupokonywa silaha wanamuqawama na kusema kuwa, makundi ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina hayajaafiki kipengele kinachohusiana na upokonyaji silaha.
-
Jinai za Marekani nchini Syria
Oct 15, 2025 05:14Marekani imekuwa nchini Syria tangu mwaka 2014 kwa kisingizio cha kupambana na ISIS na imefanya jinai nyingi nchini humo.
-
Waziri Mkuu wa zamani na mkongwe wa siasa za Kenya Raila Odinga afariki dunia akiwa matibabuni India
Oct 15, 2025 04:27Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga amefariki dunia leo asubuhi huko Koothattukulam, wilayani Ernakulam nchini India, baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati anafanya matembezi yake ya kila asubuhi.
-
Kwa nini makundi ya Palestina yanakichukulia Kikao cha Sharm el-Sheikh kuwa kisicho na maana?
Oct 15, 2025 04:14Harakati ya Hamas imetoa tamko bila kutilia maanani mkutano wa kilele wa "Sharm al-Sheikh" ikisisitiza udharura wa kuzingatiwa haki halali za Wapalestina.
-
Iran: Trump hawezi kuwa mtu wa kuleta amani wakati anachochea vita visivyo na mwisho
Oct 15, 2025 02:33Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi amemkosoa vikali Donald Trump kwa sera yake ya kuchochea vita katika eneo la Asia Magharibi, akisema rais wa Marekani hawezi kudai anapigania kuleta amani katika eneo hili huku akifuata sera za uchokozi na kufungamana na "wahalifu wa kivita."
-
Israel yaanza ukhabithi wake, yapunguza misaada ya kuingizwa Ghaza hadi nusu, yazuia fueli kikamilifu
Oct 15, 2025 02:33Utawala wa kizayuni wa Israel umeueleza Umoja wa Mataifa kwamba, kuanzia leo Jumatano utaruhusu malori 300 tu ya misaada kwa siku, ikiwa ni nusu ya idadi iliyokubaliwa kuingia katika Ukanda wa Ghaza na kwamba hakuna mafuta yoyote au gesi itakayoruhusiwa kuingizwa katika eneo hilo isipokuwa kwa mahitaji maalumu yanayohusiana na miundombinu ya kibinadamu.
-
Afrika Kusini: Kesi ya mauaji ya kimbari tuliyofungua ICJ dhidi ya Israel itaendelea licha ya vita kusitishwa
Oct 15, 2025 02:32Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema usitishaji vita wa Ghaza hautaathiri kesi ya mauaji ya kimbari iliyofunguliwa na nchi yake dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).
-
Mahakama ya Madagascar "yamwita" kanali wa jeshi akachukue uongozi na kuitisha uchaguzi
Oct 15, 2025 02:32Mahakama ya Juu ya Katiba ya Madagascar jana Jumanne "ilimwita" kamanda wa Kituo cha Uendeshaji cha Wafanyakazi wa Jeshi (CAPSAT) Kanali Michael Randrianirina "akatekeleze kazi za mkuu wa nchi."
-
Chama cha rais wa Gabon chapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Bunge
Oct 15, 2025 02:31Chama tawala cha Rais wa Gabon Brice Oligui Nguema, cha Muungano wa Kidemokrasia wa Wajenzi (Democratic Union of Builders) (UDB) kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Bunge, kwa kunyakua viti 102 kati ya 145 baada ya kutangazwa matokeo ya duru ya kwanza na ya pili ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika nchini humo.