-
Kiongozi wa upinzani Cameroon Issa Tchiroma Bakary ajitangaza mshindi wa kiti cha urais
Oct 14, 2025 09:16Issa Tchiroma Bakary kiongozi wa upinzani nchini Cameroon ametangaza kwa upande mmoja kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa juzi Jumapili akimbwaga mshindani wake mkuu Rais Paul Biya ambaye amekuwa madarakani Cameroon kwa miaka 43.
-
Iran: Trump hana haki ya kuzungumzia amani wakati anaisaidia Israel kuua watu kwa umati
Oct 14, 2025 02:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imejibu matamshi ya kibazazi ya Trump dhidi ya Tehran wakati alipolihutubia Bunge la Israel Knesset na imesema kuwa, Marekani ndiye nchi mzalishaji mkubwa wa ugaidi duniani na muungaji mkono mkuu wa wa utawala wa kigaidi umaofanya mauaji ya umati huko Ghaza, vipi inajipa mamlaka ya kimaadili ya kuwatuhumu watu wengine? Taarifa hiyo imesema kamwe wananchi wa Iran hawatasamehe wala kusahau jinai ya kinyama ya Marekani dhidi yao.
-
Jihadul Islami yaupongeza Muqawama kwa kushikamana mpaka kuachiliwa kihistoria mateka wa Palestina
Oct 14, 2025 02:51Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Jihadul Islami ya Palestina imepongeza kuachiliwa huru mateka wa Palestina katika jela za kuogofya za kutokana na ushujaa wa wamamapambano wa kambi ya Muqawama na nguvu za mshikamano na umoja wa kitaifa wa Wapalestina.
-
Harakati ya Ukombozi wa Palestina: Hakuna mazungumzo yoyote kuhusu silaha
Oct 14, 2025 02:51Utawala wa Kizayuni mara kwa mara umekuwa ukipiga ngoma ya kuwapokonya silaha wananchi wa Ghaza na hilo imelifanya zaidi wakati wa vita vyake vya miaka miwili dhidi ya Ghaza, lakini hatimaye umelazimika kusalimu amri mbele ya Muqawama na mbele ya silaha za Wapalestina. Umekubali kusimamisha vita hivyo ili kubadilishana mateka, baada ya kushindwa kuwakomboa mateka hao kwa njia za kijeshi.
-
Medvedev: Vita vitaendelea hadi taifa la Palestina litakapoundwa na kutambuliwa duniani
Oct 14, 2025 02:50Rais wa zamani wa Russia, Dmitry Medvedev, amesisitizia haja ya kuundwa taifa huru la Palestina na kutambuliwa uwepo wa nchi huru ya Palestina duniani akisema kuwa, vita haviwezi kumalizika ila kwa kuundwa nchi huru ya Palestina.
-
Mkutano wa G20 kuhusu mazingira waanza kufanyika nchini Afrika Kusini
Oct 14, 2025 02:50Mkutano wa Tatu na G20 wa mwisho wa Kikosi Kazi cha Mazingira na Ulinzi Endelevu wa Hali ya Hewa (ECSWG) ulifunguliwa rasmi jana Jumatatu mjini Cape Town, Afrika Kusini.
-
Ndoto ya ushindi; mzozo mpya katika siasa za ndani za Israel baada ya makubaliano ya amani
Oct 14, 2025 02:44Makubaliano ya amani ya Trump, licha ya madai ya Netanyahu kuwa ni "ushindi," yamewakasirisha Wazayuni wengi.
-
Watumiaji wa X: Hamas imehuisha jina Palestina/ Israel ndilo neno linalochukiwa zaidi duniani
Oct 14, 2025 00:55Katika radiamali kwa makubaliano ya kuhitimisha vita huko Gaza, watumiaji wa mtandao wa kijamii wa "X" wamesema utawala wa Kizayuni umeshindwa kufikia malengo yake dhidi ya muqawama wa Kiislamu wa Palestina, "Hamas."
-
Ushindi kwa HAMAS: Mamia ya mateka wa Kipalestina waachiliwa huru
Oct 14, 2025 00:35Mamia ya mateka wa Kipalestina wameachiliwa huru kutoka jela za Israel siku ya Jumatatu chini ya awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza. Katika uamuzi wa kushangaza jeshi la Israel limetoa onyo dhidi ya kusherehekea hadharani Wapalestina kuachiliwa huru ndugu zao.
-
Baadhi ya ripoti: Rais wa Madagascar ametorokea Ufaransa
Oct 14, 2025 00:23Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa Rais Andry Rajoelina wa Madagascar ameikimbia nchi hiyo na kuelekea Ufaransa.