-
Kwa nini mwenendo wa kukabiliana na sarafu ya dola umeshika kasi duniani?
Oct 13, 2025 23:06Hisa ya sarafu ya Yuan ya China katika malipo ya biashara na upokeaji imefikia takriban 53%, na kuipita hisa ya dola ya 47%. Mabadiliko haya ya kihistoria yanakuja katika hali ambayo mwaka 2010 hisa ya Yuan katika biashara ya nje ya China takribani ilikuwa sifuri.
-
Jeshi la Kizayuni lilichoma moto majengo na chakula kabla ya kukimbia Ghaza
Oct 13, 2025 22:58Tovuti ya Drop Site News, chombo cha habari cha uchunguzi kilichoko Washington kimefichua kuwa, jeshi la Israel lilichoma kinyama nyumba na vyakula kabla ya kukimbia Ukanda wa Ghaza na baadaye kusambaza picha za unyama huo kwa majivuno na kiburi kikubwa kwenye mitandao ya kijamii.
-
Jeshi la Sudan ladai kuua zaidi ya wapiganaji 100 wa RSF magharibi mwa nchi
Oct 13, 2025 22:58Jeshi la Sudan (SAF) limetoa taarifa na kudai kuwa, zaidi ya wapiganaji 100 wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) wameuawa katika mapigano ya El Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini huko magharibi mwa Sudan.
-
Islamabad: Operesheni ya Taliban dhidi ya Pakistan ilifanywa kwa uratibu na India
Oct 13, 2025 22:57Waziri wa habari wa Pakistan, amezungumzia mzozo wa mpaka wa nchi yake na Afghanistan, akidai kuwa operesheni hiyo ilifanywa kwa uratibu na India na kwamba shambulio hilo lilikuwa sehemu ya operesheni ya India inayojulikana kwa jina la Sindoor.
-
Kushindwa utawala wa kizayuni Ghaza; ushindi wa Muqawama katika medani ya vita na kwenye ulingo wa siasa
Oct 13, 2025 22:55Makundi ya Muqawama wa Palestina yanasisitiza kutekelezwa matakwa yao halali na ya wananchi wa Palestina katika makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
Iran: Dunia iwe macho, isikubali Israel ikiuke usitishaji vita Gaza
Oct 13, 2025 08:47Iran imesisitiza uungaji mkono wake usioyumba kwa juhudi zozote zinazolenga kukomesha mauaji na mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza, ikionya kuhusu historia ya utawala unaoikalia kwa mabavu Quds ya kukanyaga mikataba na makubaliano.
-
Ulimwengu wa Spoti, Okt 13
Oct 13, 2025 08:21Ufuatao ni mkusanyiko wa matukio yaliyotifua mavumbi viwanjani ndani ya siku zilizopita duniani, kuanzia hapa Iran hadi barani Afrika.
-
Mali yajibu mapigo, yawawekea Wamarekani vikwazo
Oct 13, 2025 07:59Serikali ya Mali imeweka masharti ya bondi ya viza kwa raia wa Marekani, ili kulipiza kisasi cha uamuzi wa Washington wa kuwawekea vikwazo vya usafiri raia wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
-
AU yampongeza Patrick Herminie kwa kushinda urais Ushelisheli
Oct 13, 2025 06:41Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) Mahmoud Ali Youssouf amempongeza Patrick Herminie kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Ushelisheli.
-
Hamas yaonya; Israel inaendelea kuchuja orodha ya mateka
Oct 13, 2025 06:12Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas kuushutumu utawala ghasibu wa Israel kwa 'kutia mkono' orodha ya mateka wa Kipalestina, na kukwepa kutekelezwa masharti na vipengee vya makubaliano ya usitishaji vita Gaza, licha ya ahadi zake kwa wapatanishi wa kimataifa.