Ulimwengu wa Spoti, Okt 13
Ufuatao ni mkusanyiko wa matukio yaliyotifua mavumbi viwanjani ndani ya siku zilizopita duniani, kuanzia hapa Iran hadi barani Afrika.
Mieleka ya Pahlevani: Iran kidedea
Iran ilishinda taji la Mashindano ya Mieleka ya Asia ya 2025 ya Pahlevani siku ya Ijumaa. Wanamieleka hao wa Iran walishinda medali nne za dhahabu pamoja na medali ya fedha. Mehdi Veisi alishinda medali ya dhahabu katika uzani wa kilo 60 baada ya kumshinda mpinzani wake Mhindi. Rahman Rahimpour alinyakua dhahabu ya pili, na kumshinda mpinzani wake wa Kihindi katika kilo 70. Abdollah Sheikh Azami alishinda dhahabu katika kilo 80, akimshinda mwanamieleka kutoka Kyrgyzstan.

Naye Alireza Sahraei alitwaa dhahabu ya nne ya Iran katika kilo 90 kwa kumshinda mpinzani wake wa Kirgizia. Aidha Mostafa Najafi alishindwa na mwanamieleka wa Iraq katika pambano la mwisho la +90kg. Mashindano hayo yalifanyika Urmia, Iran kwa kushirikisha wanamieleka 180 kutoka nchi 17.
Unyanyuaji uzani: Iran bingwa
Timu ya wanaume ya Iran ya kunyanyua vitu vizito imeibuka kidedea katika Mashindano ya Dunia ya Kunyanyua Uzani ya 2025, yaliyofanyika mjini Førde, Norway, kuanzia Oktoba 2 hadi 11. Iran iliyowashirikisha Abdollah Beiranvand, Ilya Salehipour, Alireza Moeini, Ali Alipour, Abolfazl Zare, Ayat Sharifi na Ali Davoudi - ilijizolea medali moja ya dhahabu, nne za fedha na moja ya shaba, na kumaliza na jumla ya pointi 388 na kutwaa ubingwa. Korea Kaskazini na Marekani zilimaliza za pili na tatu mtawalia. Timu ya Iran, inayoongozwa na kocha mkuu Behdad Salimi, ilitwaa ubingwa wa timu ya dunia kwa mara ya pili katika historia yake. Kufuatia ushindi huo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Aref katika ujumbe wake wa tahania amelipongeza taifa la Iran kwa kuipaisha Iran, akieleza kuwa serikali na taifa hili linajivunia ushujaa na ubingwa huo.

Wakati huo huo, Atiyeh Sadat Hosseini ameingia kwenye madaftari ya historia baada ya kushinda medali ya dhahabu ya kwanza kabisa kwa wanawake wa Iran katika Mashindano ya Dunia ya Kunyayua Uzani ya Walemavu, kwa kuibuka kidedea katika kitengo cha kilo 61 kwa wanawake. Haya yalikuwa Mashindano makubwa zaidi kuwahi kutokea ya Rookie & Next Gen ya Dunia yenye wanamichezo 120 (36 wa kike na 84 wa kiume), wenye umri wa chini ya miaka 20, walishiriki katika matukio 19 yaliyochukua muda wa siku mbili. Duru hii itafuatiwa na Mashindano ya Dunia ya Wasomi, yatakayofanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 18 - ikiwa ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kuandaliwa sio tu nchini Misri bali pia barani Afrika. Pia ni miongoni mwa michuano mikubwa zaidi kuwahi kufanyika nchini Misri, kufuatia michuano ya wazi ya Afrika mwaka 2022 na Kombe la Dunia mwaka 2023 na 2024.
Hali kadhalika, Hadi Choopan wa Iran alishika nafasi ya pili katika shindano la 2025 la kututumua misuli la Mr. Olympia kwa upande wa wanaume. Mmarekani Derek Lunsford imetwaa nafasi ya kwanza na kutunkiwa $600,000); huku Hadi Choopan akizawadiwa $200,000.

Polo Fainali; Iran yaibuka ya 2
Timu ya Iran ya mchezo wa polo ya majini ya Iran ilishindwa na China kwa mabao 16-15 siku ya Jumamosi katika mechi ya fainali ya Mashindano ya Polo ya Asia ya 2025. Mechi hiyo ilienda kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 11-11 na chine kuibuka kidedea kwa mabao 5-4. Timu ya Melli ilishinda Uchina (14-9), Hong Kong (22-10), Uzbekistan (28-7), Thailand (21-6), na Japan (19-18) katika shindano hilo. Iran itacheza na mshindi wa China na Kazakhstan katika mechi ya fainali siku ya Jumamosi.

Mashindano ya 11 ya Aquatics ya Asia yatafanyika kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 11 kwenye Uwanja wa Veer Savarkar Sports mjini Ahmedabad, India. Mashindano ya 11 ya Aquatics ya Asia yatafanyika kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 11 huko Ahmedabad, India.
Iran yapongezwa kwa kung'ara India
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameipongeza timu ya wanariadha wa Jamhuri ya Kiislamu kwa kumaliza katika nafasi ya tatu katika Duru ya 12 ya Mashindano ya Riadha ya Walemavu yaliyofanyika nchini India. Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa, uanamichezo na kuakisi utamaduni wa Kiislamu wa Iran kunazipa thamani kubwa medali za wanariadha wa nchi hii, na wanatazamiwa kung'ara zaidi katika duru ijayo ya Michezo ya Mshikamano wa Kiislamu mjini Riyadh. Wanamichezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameng'ara kwenye mashindano hayo ya kimataifa kwa kujinyakulia medali tisa za dhahabu, mbili za fedha na tano za shaba katika michezo tofauti ikiwemo kurush tufe, kisahani, na mshale. Brazil iliongoza jedwali la medali kwa kuzoa medali 44 (15 za dhahabu, 20 za fedha, 9 za shaba). China iliambulia dhahabu 13, fedha 22, na shaba 17 (jumla ya medali 52) lakini ilimaliza ya pili kutokana na kuwa na dhahabu mbili pungufu, nyuma ya Brazil.
Soka: Iran yanyukwa na Russia
Timu ya kandanda ya Russia iliitandika Iran mabao 2-1 katika mechi ya kirafiki iliyofanyika katika uwanja wa Volgograd Arena Ijumaa usiku. Dmitri Vorobyov alipokea mpira kutoka kwa Anton Miranchuk dakika ya 22 na kuunawa mpira juu ya kichwa cha Alireza Beiranvand na kuongoza Russia. Dakika tatu baada ya kipindi cha pili kuanza, Amirhossein Hosseinzadeh, aliyesaidiwa na Saman Ghoddos, alisawazisha bao hilo. Kikosi cha Valery Karpin kiliiweka Iran chini ya shinikizo na kutengeneza nafasi nyingi mbele ya mashabiki 43,000 kwenye uwanja. Aleksey Batrakov anayetumia mguu wa kulia alifungua bao la Beiranvand kutoka eneo la nje katika dakika ya 70. Timu hiyo ya soka ya Iran inayofahamika hapa nchini kama Timu Melli itacheza na Tanzania Jumanne huko Dubai, nchini Imarati.
Fainali Ngao ya Jamii Wanawake: Simba Queens vs JKT Queens
Nani malkia wa soka nchini Tanzania? Ndilo swali ambalo lilikuwa linawaumiza wengi vichwa kabla ya mchuano wa Jumapili wa fainali ya Ngao ya Jamii uliowakutanisha Simba Queens na JKT Queens. Na ni wazi sasa kuwa JKT Queens imebeba taji hilo lwa mara ya pili mfululizo, baada ya kuichaza mabanati wa Simba mabao 2-1 katika mhezo uliopigwa Jumapili katika Uwanja wa KMC. Bao la Winfrida Gerald dakika ya 12 na lile la Simba walilojifunga la winga Asha Omary dakika ya 17 liliipa timu hiyo taji la pili la mashindano hayo na lile la kufutia machozi la Wanamsimbazi likifungwa na Zawadi Usanase. JKT Queens kwa sasa inaendelea kujiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake inayotarajiwa kuanza mapema Novemba nchini Algeria. Timu hiyo ilipata nafasi ya kushiriki michuano hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Mbio za Kombe la Dunia 2026; Algeria yatinga
Algeria imekuwa nchi ya nne ya Afrika kutinga fainali za Kombe la Dunia za 2026. Riyad Mahrez aliongoza kutoka mbele huku Algeria ikiwa taifa la nne la Afrika kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026 baada ya kuichabanga timu chovu ya Somalia mabao 3-0. Winga huyo wa zamani wa Manchester City na Leicester City alitoa krosi kwa bao la mapema la Mohamed Amoura na kisha akajifunga mwenyewe katika dakika ya 19. Mahrez, ambaye alikuwa nahodha wa timu yake, alicheza na mfungaji wake kabla ya kutengeneza la tatu kwa Amoura dakika 12 kipindi cha pili, na wote wawili wakatolewa muda mfupi baadaye. Mbweha hao wa Jangwani wamehakikishiwa nafasi ya kwanza katika Kundi G wakiwa wamebakisha mchezo mmoja na watarejea Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 2014, walipofungwa na mabingwa Ujerumani katika hatua ya 16 bora. Mchezo huo ulikuwa wa nyumbani kwa Somalia, lakini ulipigwa katika mji wa pwani wa Algeria kwa sababu Ocean Stars hawana uwanja unaofaa kwa soka la kimataifa nchini mwao.

Vijana wa Vladimir Petkovic wanaungana na timu za Afrika Kaskazini Morocco, Tunisia na Misri kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazororoma Amerika Kaskazini na Kati. Kwa upande wake, Uganda ambayo ipo katika nafasi ya pili katika Kundi G, ilifufu matumainiyake ya kutinga fainali hizo baada ya kuilaza Botswana 1-0. Bao hilo la The Cranes lilifungwa na Jude Ssemugabi aliyefunga kwa kichwa kipindi cha pili kutoka kona, katika mchezo wa ugenini uliopigwa Alkhamisi katika Uwanja wa Obed Itani Chilume jijini Francistown. The Cranes wako pointi tatu mbele ya Msumbiji, ambao walinyukwa mabao 2-1 nyumbani walipovaana na Guinea, na wana faida ya mabao 10 dhidi ya wapinzani wao linapokuja suala la tofauti ya mabao. Huku hayo yakiarifiwa, mchezo mwingine wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 kati ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Zambia ‘Chipolopolo’ uliofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar uliishia kwa Stars kunyukwa bao moja bila jibu. Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu, Taifa Stars, imekubali kichapo hicho laini katika mchezo uliopigwa Oktoba 8 huko visiwani. Katika mchezo huo, Zambia walipata bao pekee kupitia kwa mchezaji wao Fashion Sakala katika dakika ya 75 ya mchezo. Kwa matokeo hayo, Taifa Stars inasalia na pointi 10, ikishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi E. Morocco inaongoza kundi hilo kwa alama 21, ikifuatiwa na Niger yenye pointi 12. Wakati huo huo, Harambee Stars ya Kenya iliibanjua Burundi bao 1-0 katika mchuano wake wa kusaka tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia. Katika mchezo huo uliopigwa Alkhamisi ya Oktoba 9 katika Uwanja wa Intwari jijini Bujumbura, Stars waliutandaza mpira na kuwapeleka msobemsobe wenyeji. Bao la pekee na la ushindi kwenye mchezo huo ulifungwa na nyota Stars, Ryan Ogam. Kwingineko siku ya Alkhamisi, Liberia iliweka hai matumaini ya kumaliza katika nafasi ya pili katika Kundi H kwa ushindi wa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Namibia. Katika matokeo mengine ya michuano ya kusaka tiketi za Kombe la Dunia 2026, Gabon iliizaba Gambia mabao 4-3 katika mchezo uliopigwa Ijumaa katika Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi. Gabon itahitaji upendeleo mkubwa kutoka kwa Harambee Stars ya Kenya, ambayo itavaana na Ivory Coast mjini Abidjan katika mchezo wao wa mwisho wa kundi Jumanne.
Israel yanyukwa na kuzomewa uwanjani
Erling Haaland alifunga mabao 3 ya hat-trick na kufikisha jumla ya magoli 50 ya kimataifa katika muda wa rekodi, wakati Norway ikiisagasaga Israel kwa kuigaragaza mabao 5-0, na kukaribia kufuzu kwa fainali za kwanza za Kombe la Dunia la FIFA tangu 1998. Kabla ya mechi hiyo ya Jumamosi usiku huko Oslo, mamia ya watu walihudhuria maandamano ya wafuasi na waungaji mkono wa Palestina, wakipiga nara za "Palestina Huru" kupinga "mauaji ya kimbari" ya Israel huko Gaza. Polisi wa Norway walitawanya mkusanyiko wa wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina kwa kutumia mabomu ya gesi ya kutoa machozi na kuwatia mbaroni watu kadhaa. Wakati huo huo, ushiriki wa timu utawala wa kizayuni wa Israel umefutwa katika mashindano ya Dunia ya Jimnastiki ya Jakarta Indonesia kulalamikia jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Katika taarifa yake ya mshikamano na watu wa Gaza, serikali ya Indonesia imefuta ushiriki wa timu ya Israel ya Jimnastiki katika Mashindano ya Dunia ya Gymnastics mjini Jakarta na kutangaza kuwa haitatoa visa ya kuingia kwa wanariadha kutoka Israel.

Wizara ya Sheria na Haki za Binadamu ya Indonesia imetoa taarifa na kutangaza kwamba, hakuna mjumbe auu mwakilishi wa michezo wa Israel atakayepewa visa ya kushiriki Mashindano ya Dunia ya Jimnastiki, ambayo yamepangwa kufanyika mjini Jakarta kuanzia Oktoba 19 hadi 25. Akifafanua kuhusiana na uamuzi huo, Yusril Ihza Mahendra Waziri wa Sheria na Haki za Bibinadamu wa Indonesia amesema: "Indonesia inazingatia sera yake ya muda mrefu; hakuna uhusiano wowote na Israel utakaoanzishwa hadi pale utawala huo utakapolitambua taifa huru la Palestina." Mashabiki wa soka katika nchi mbali mbali duniani zikiwemo za Ulaya wamejiunga na kampeni ya 'Show Israel Red Card' yaani "Ionyeshe Israel Kadi Nyekundu" katika viwanja wa soka ili kuonyesha uungaji mkono wao kwa Palestina na kulaani jinai za Wazayuni katika Ukanda wa Gaza.
…………………MWISHO…..………..