-
Ajali ya basi yaua watu 42 nchini Afrika Kusini
Oct 13, 2025 05:59Watu wasiopungua 42 wamepoteza maisha baada ya basi walilokuwa wakisafiria kubingiria katika jimbo la Limpopo, kaskazini mwa Afrika Kusini.
-
Hamas yawakabidhi kwa Msalaba Mwekundu huko Gaza mateka 7 wa kwanza wa Israel
Oct 13, 2025 03:10Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (ICRC) limetangaza kukabidhiwa mateka saba wa kwanza wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Ripoti: Iran yauza bidhaa za kilimo katika nchi 80 duniani
Oct 13, 2025 02:56Imeelezwa kuwa, mazao ya kilimo ya Iran yanasafirishwa kwenda nchi 80 duniani. Kwa kurekodi ukuaji mkubwa wa uzalishaji wa kilimo, Iran imejitambulisha kama mmoja wa wahusika wakuu katika soko la chakula la kimataifa.
-
UNICEF: Watoto 56,000 wamebaki yatima Gaza kutokana na vita vya Israel
Oct 13, 2025 02:55Mfuko wa Kuhudumia Watoto Umoja wa Mataifa wa (UNICEF) umetangaza kuwa, watoto 56,000 katika Ukanda wa Gaza wamebaki mayatima baada ya kupoteza mzazi mmoja au wote wawili katika kipindi cha miaka miwili ya vita vya jeshi la Israel katika uukanda huo.
-
Waislamu wa Nigeria washerehekea usitishaji vita Gaza
Oct 13, 2025 02:54Wanachama wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria katika Jimbo la Bauchi wamesherehekea makubaliano ya kusitisha vita Gaza, ambayo yanaruhusu maelfu ya watu kurejea kwenye nyumba zao zilizobomolewa katika ukanda wa Gaza, kuondolewa kwa vikosi vya mauaji ya halaiki ya Israel na kubadilishana mateka.
-
Mabinti barani Afrika watoa wito wa kuheshimiwa haki zao
Oct 13, 2025 02:54Mabinti barani Afrika wametoa mwito wa kuheshimiwa na kupatiwa kipaumbele haki zao za kimsingi. Wito huo umetolewa katika kongamano la kieneo la mabinti magharibi mwa Afrika. Imeelezwa kuwa, haki za mabinti Afrika ni sauti ambayo haiwezi tena kupuuzwa.
-
Iran yakataa mwaliko wa mkutano wa Gaza; yasema haiwezi kuketi meza moja na walioishambulia
Oct 12, 2025 23:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekataa mwaliko uliotolewa kwa Tehran kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano kuhusu Gaza uliopangwa kufanyika huko Sharm el Sheikh, Misri akisema kuwa hawezi kuketi pamoja na viongozi waliowashambulia wananchi wa Iran na wanaoendelea kuitishia nchi hii na kuiwekea vikwazo.
-
AU yataka pande hasimu Madagascar kustahamiliana na kufungua mlango wa mazungumzo
Oct 12, 2025 22:58Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) Mahmoud Ali Youssouf jana Jumapili alizitaka pande zinazozozana nchini Madagascar kujizuia na kuvulimiana ili kufungua mlango wa mazungumzo wa kutatuliwa kisiasa mvutano uliozuka nchini humo.
-
Serikali ya Sudan: Waasi wa RSF wameua raia 57 wengine El Fasher
Oct 12, 2025 22:57Serikali ya Sudan imetangaza kwamba shambulizi la droni na ndege zisizo na rubani za Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF limeua raia 57 katika makazi yao ya muda ya mji wa El Fasher wa magharibi mwa Sudan.
-
Ansarullah yaipa muda Israel kuhakikisha inatekeleza kikamilifu usitishaji vita Ghaza
Oct 12, 2025 22:57Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ameupa utawala wa Kizayuini muda maalumu wa kuhakikisha unaheshimu na kutekeleza makubaliano ya kusimamisha vita vinginevyo Yemen itaanzisha tena operesheni za kijeshi dhidi ya Israel.