Ripoti: Iran yauza bidhaa za kilimo katika nchi 80 duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i131932-ripoti_iran_yauza_bidhaa_za_kilimo_katika_nchi_80_duniani
Imeelezwa kuwa, mazao ya kilimo ya Iran yanasafirishwa kwenda nchi 80 duniani. Kwa kurekodi ukuaji mkubwa wa uzalishaji wa kilimo, Iran imejitambulisha kama mmoja wa wahusika wakuu katika soko la chakula la kimataifa.
(last modified 2025-10-13T11:53:10+00:00 )
Oct 13, 2025 06:26 UTC
  • Ripoti: Iran yauza bidhaa za kilimo katika nchi 80 duniani

Imeelezwa kuwa, mazao ya kilimo ya Iran yanasafirishwa kwenda nchi 80 duniani. Kwa kurekodi ukuaji mkubwa wa uzalishaji wa kilimo, Iran imejitambulisha kama mmoja wa wahusika wakuu katika soko la chakula la kimataifa.

Wizara ya Jihadi ya Kilimo ya Iran imetangaza katika ripoti yake kwamba: Uzalishaji wa kilimo wa Iran umefikia tani milioni 125 na bidhaa hizo zinasafirishwa kwenda katika nchi zaidi ya 80 duniani.

" Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Iran ni miongoni mwa nchi 14 zinazoongoza kwa uzalishaji wa ngano duniani na ni miongoni mwa nchi 10 duniani kwa uzalishaji wa kuku na mayai.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Asia Magharibi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Biashara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Mauzo ya Iran nje ya nchi yameongezeka katika nusu ya kwanza ya mwaka huu kwa nchi za eneo zikiwemo Uturuki, Qatar, Oman na Bahrain.

Abdol Amir Rabihavi, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Magharibi mwa Asia ya Shirika la Maendeleo ya Biashara la Iran amesema: Mauzo ya nje katika nchi za Asia Magharibi zikiwemo Uturuki, Qatar, Oman na Bahrain yameshuhudia ongezeko la asilimia 8 hadi 9 katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu.

Ukuaji wa biashara ya Iran na mataifa mengine unashuhudiwa katika hali ambayo, katika miaka ya hivi karibuni taifa hili limekuwa likiandamwa na vikwazo vya kidhalimu vya Marekani na washirika wake.