Yemen yahimiza msimamo mmoja wa Ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i131984-yemen_yahimiza_msimamo_mmoja_wa_ulimwengu_wa_kiislamu_dhidi_ya_israel
Serikali ya Yemen imethibitisha uungaji mkono wake kwa watu wa Gaza kufuatia kutekelezwa makubaliano ya kusitisha vita kati ya Hamas na Israel.
(last modified 2025-10-14T12:48:53+00:00 )
Oct 14, 2025 12:48 UTC
  • Yemen yahimiza msimamo mmoja wa Ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya Israel

Serikali ya Yemen imethibitisha uungaji mkono wake kwa watu wa Gaza kufuatia kutekelezwa makubaliano ya kusitisha vita kati ya Hamas na Israel.

Mahdi al Mashat Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen ameeleza haya katika hotuba kwa mnasaba wa maadhimo ya mwaka wa 62 wa mapinduzi ya Yemen. 

Mashat amezitolea wito nchi za Kiarabu na Kiislamu kudhidhirisha msimamo wa pamoja kupingwa ukiukaji unaofanywa na Israel dhidi ya nchi za kanda hii. Amesema, Yemen itaendelea kufuatilia kwa makini na kwa karibu utekelezaji wa makubaliano ya kusimamisha vita na utumaji wa misaada ya kibinadamu huko Gaza. 

Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amewapongeza wale wote waliojitolea bega kwa bega kuwasaidia wananchi madhulumu wa Palestina khususan Harakati ya Hizbullah ya Lebanon na pia wananchi wa Iraq na Iran. 

Mashat amezishukuru nchi zote zilizoamua kuvunja uhusiano na Israel au kuuwekea utawala huo vikwazo. 

"Tutafanya kazi kukuza na kuendeleza uwezo wetu wa kijeshi katika nyanja zote ili kutuwezesha kukabiliana na teknolojia zote za kisasa za kijeshi za adui," amesema Mahdi al Mashat.

MNkuu huyo wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vitaendelea kuilinda Yemen hadi kukombolewa kila shibri ya ardhi ya Jamhuri ya Yemen.