Oct 14, 2023 13:37 UTC
  • Mwanajeshi Mzayuni atoa amri ya kuuliwa Waarabu wote + VIDEO

Duru za Kizayuni zimesambaza mkanda wa video unaomuonesha mwanajeshi mmoja Mzayuni akitoa amri kwa wanajeshi wenzake na Wazayuni kwa ujumla kuhakikisha wanawaua Waarabu wote na wasimbakishe hata mtoto mdogo.

Mkanda huo wa video ulioenea kwenye mitandao ya kijamii umezusha makelele mengi na umezidi kuwathibitishia walimwengu ukatili wa kupindukia wa Wazayuni.

Afisa huyo mstaafu wa jeshi katili la Israel, mwenye umri wa miaka 95 anasikika katika mkanda huo wa video akiwaamrisha Wazayuni  wasimbakishe hai Mwarabu yeyote. Anasikika akisema: Msibakishe Mwarabu hata mmoja! Wasafisheni kabisa katika uso wa dunia! Kama jirani yako ni Mwarabu nenda sasa hivi ukamuue!

Vile vile anasikikia akiwaambia wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni kwamba: Rudini na ushindi. Nendeni mkawamalize kabisa. Msibakishe hai hata mmoja. Futeni kumbukumbu zao duniani. Wafuteni kabisa. Familia zao, mama zao, watoto wao, wanyama hao wote hawapaswi kubakishwa hai zaidi ya hivi sasa.

Mwanajeshi huyo wa Israel anaendelea kutoa matamshi yake ya kijinai akisema: Leo hakuna kisingizio chochote cha kutuzuia kufanya tunalotaka. Huenda kesho Hizbullah ikaanzisha mashambulio ya anga dhidi yetu. Huenda Waarabu waliopo hapa nao wakatushambulia. Kila Myahudi mwenye silaha lazima aende kuwaua Waarabu.

Aidha anasikika akisema: Kama una jirani Mwarabu, usisite hata chembe, nenda nyumbani kwake na mpige risasi. Washambulieni, msisubiri wakushambulieni.

Matamshi ya Mzayuni huyo yanaonesha ni kiasi gani alivyo na roho ya kikatili kama Wazayuni wenzake na ni namna gani alivyokuwa akifanya jinai dhidi ya Wapalestina na dhidi ya Waarabu wakati alipokuwa anahudumu jeshini.

Matamshi hayo ya chuki na jinai ya mwanajeshi wa Israel yanaendelea kulaaniwa katika kona mbalimbali za dunia na walimwengu wanazidi kuona ni jinsi gani utawala wa Kizayuni ulivyo na ukatili wa kuchupa mipaka.