-
Answarullah yakadhibisha madai ya Mohammad Bin Salman kuhusu Yemen
Mar 07, 2018 11:18Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Answarullah nchini Yemen amesema kuwa, matamshi ya Mohammad Bin Salman Al Saud, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia kwamba vita nchini Yemen vinakaribia kuisha ni uongo mtupu.
-
Komandi ya kijeshi ya Imarati yashambuliwa kwa kombora la belestiki Yemen
Feb 23, 2018 21:19Jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen zimeshambulia kwa kombora la belestiki komandi wa kijeshi ya wanajeshi vamizi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) katika mkoa wa Ma'rib nchini Yemen.
-
Wakuu wa Iran, Ansarullah wajadili suluhisho la kisiasa Yemen, utoaji misaada
Feb 13, 2018 23:22Maafisa wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Harakati ya Ansarullah ya Yemen wamefanya mazungumzo mjini Tehran kujadili njia za kuhitimisha mgogoro wa kisiasa katika nchi hiyo ya Kiarabu na udharura wa kuwaikifhsia misaada wananchi wake.
-
Answarullah: Saudia ndiye kizuizi kikubwa cha utatuzi wa mgogoro wa Yemen
Jan 29, 2018 01:07Kiongozi mmoja mwandamizi wa harakati ya wananchi ya Answarullah ya Yemen amesema kuwa, mzozo uliozuka baina ya Saudi Arabia na wenzake walioivamia Yemen ndiyo sababu kuendelea mgogoro na vita nchini humo.
-
Ansarullah ya Yemen yaionya Saudi Arabia
Jan 24, 2018 10:42Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameutahadharisha utawala wa Aal Saud na kutangaza kwamba, katika siku chache zijazo Saudia itashtukizwa na harakati hiyo.
-
Radiamali ya Ansarullah ya Yemen kwa madai ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia
Jan 17, 2018 11:43Msemaji wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ametoa matamshi akijibu msimamo usiozingatia hali halisi na wa hadaa uliodhihirishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia kuhusu Yemen.
-
Wanawake wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen wako tayari kuingia vitani dhidi ya Saudia
Jan 14, 2018 23:46Wanawake wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen jana Jumapili waliandamana kulaani hujuma za kinyama za Saudia dhidi ya raia nchini humo na kusema wako tayari kuingia vitani kukabiliana na wavamizi.
-
UN: Answarullah imefungamana na mazungumzo ya amani
Jan 12, 2018 04:23Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Yemen amesema kuwa, harakati ya wananchi ya Answarullah nchini humo imetoa taarifa ya kuheshimu na kufungamana na suala la kuanza upya mazungumzo ya amani nchini humo.
-
Ansarullah kuishambulia Somaliland ikiendelea kushirikiana na UAE dhidi yake
Dec 27, 2017 03:46Harakati ya Ansarullah ya Yemen imesema ikilazimu, itaishambulia jamhuri iliyojitangazia uhuru ya Somaliland kutokana na hatua yake ya kushirikiana na Umoja wa Falme za Kiarabu dhidi ya wapiganaji wa harakati hiyo ya Houthi.
-
Kiongozi wa Ansarullah Yemen: Wakidondosha mabomu Sanaa tutavurumisha makombora Riyadh na Abu Dhabi
Dec 20, 2017 04:34Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen Sayyed Abdul-Malik Badruddin al Houthi amesema: "Wavamizi wakidondosha mabomu mjini Sanaa nasi tutavurumisha makombora yetu Riyadh na Abu Dhabi. Kila siku Makombora ya Wayemen yanazidi kuimarika na yanaweza kulenga masafa marefu."