Answarullah yakadhibisha madai ya Mohammad Bin Salman kuhusu Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i41339-answarullah_yakadhibisha_madai_ya_mohammad_bin_salman_kuhusu_yemen
Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Answarullah nchini Yemen amesema kuwa, matamshi ya Mohammad Bin Salman Al Saud, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia kwamba vita nchini Yemen vinakaribia kuisha ni uongo mtupu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 07, 2018 14:48 UTC
  • Answarullah yakadhibisha madai ya Mohammad Bin Salman kuhusu Yemen

Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Answarullah nchini Yemen amesema kuwa, matamshi ya Mohammad Bin Salman Al Saud, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia kwamba vita nchini Yemen vinakaribia kuisha ni uongo mtupu.

Zaffullah al-Shami ameyasema hayo katika mahojiano na televisheni ya Al Jazeera ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza kwamba, matamshi ya Bin Salman kuhusu kukaribia kumalizika vita nchini Yemen ni mapya na na yasiyopaswa kuzingatiwa na kwamba mrithi huyo wa kiti cha ufalmbe ambaye pia ni waziri wa ulinzi wa Saudia anatafuta njia ya kujikwamua kutokana na kinamasi alichokwama ndani yake kupitia vita hivyo alivyovianzisha dhidi ya Yemen.

Zaffullah al-Shami, Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Answarullah nchini Yemen

Al-Shami ameongeza kuwa, utatuzi wa vita vya Yemen unategemea usitishaji vita wa Saudia na kwamba Wayemen wataendelea kusimama imara dhidi ya aina yoyote ya hujuma na mauaji yanayofanywa na muungano vamizi wa Saudia dhidi ya taifa lao. Mjumbe huyo wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Answarullah nchini Yemen amesema kuwa hivi sasa raia wa Yemen wako macho zaidi na njama za wavamizi wa utawala wa Aal-Saud na kwa hilo wamesimama imara na kamwe hawawezi kuhadaika au kuogopa vitisho vya utawala huo. Amesisitiza kwamba, njama za Saudia haziwezi kudhoofisha azma ya Wayemen na kuongeza kuwa, hawatojisalimisha ili kufikia amani,. 

Answarullah wakiwa wamezuia njama zote chafu za Saudia na jeshi lake nchini Yemen

Akiwa mjini Cairo, Misri Mohammad Bin Salman Al Saud, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia alidai kuwa, vita vya Yemen vinakaribia kufikia tamati kwa kuirejesha madarakani serikali ya Abdrabbuh Mansur Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutoroka nchi,  kwa kile alichosema eti ni baada ya kuidhoofisha harakati ya Answarullah. Hii ni katika hali ambayo, kinyume na madai ya Bin Salman, hadi sasa kibaraka wao huyo (Abdrabbuh Mansur Hadi) hajaweza kurejea Sana'a kama ambavyo harakati ya Answarullah imezidi kupata uungaji mkono wa Wayemen huku ikiwa ndiyo inadhibiti hali ya mambo nchini humo.