-
Bahrain yawapokonya uraia wapinzani 115, yawafunga jela maisha 53 miongoni mwao
May 15, 2018 09:27Katika kile kinachoonekana ni muendelezo wa ukandamizaji na mbinyo dhidi ya wapinzani na wakosoaji wa serikali, utawala wa Aal-Khalifa umewavua uraia wananchi 115 wa Bahrain, huku ukiwahukumu kifungo cha maisha jela 53 miongoni mwao.
-
Associated Press lafichua: Nentayahu alionana na mabalozi wa UAE na Bahrain, Washington
May 13, 2018 11:12Shirika la habari la Associated Press limefichua kuwa Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu alikutana na mabalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain nchini Marekani mnamo mwezi Machi mwaka huu, hatua inayozidi kuweka wazi uhusiano mzuri uliopo kati ya Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu.
-
Imarati na Bahrain kushiriki sherehe za miaka 70 ya kuundwa utawala pandikizi wa Israel
May 03, 2018 23:38Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) zimetangaza kuwa zitashiriki katika mashindano ya pikipiki yaliyoitishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel yanayoanza leo Ijumaa.
-
Radiamali ya watu wa Bahrain dhidi ya hukumu za kifo dhidi ya wapinzani
Apr 26, 2018 21:57Kufuatia kutolewa hukumu ya kifo dhidi ya vijana sita wa Bahrain na mahakamu ya kijeshi ya Aal Khalifa, Wabahrain wameandamana katika pembe tofauti za nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi kulalamikia ukandamizaji wa utawala huo dhidi yao.
-
Utawala wa Bahrain wawahukumu watu sita adhabu ya kifo kwa tuhuma bandia
Apr 25, 2018 23:16Mahkama ya rufaa ya kijeshi nchini Bahrain, imetoa hukumu ya adhabu ya kifo dhidi ya raia sita wa nchi hiyo kwa tuhuma bandia kwamba walijaribu kupanga shambulizi dhidi ya kamanda wa vikosi vya ulinzi nchini humo.
-
Al Wifaq: Polisi wa Bahrain wameshadidisha mzingiro dhidi ya nyumba ya Sheikh Isa Qassim
Apr 13, 2018 02:37Jumuiya ya Kiislamu ya al Wifaq ya nchini Bahrain imetangaza kwamba utawala wa kidikteta wa Aal Khalifa nchini humo umezidisha mzingiro dhidi ya nyumba ya mwanazuoni mkubwa wa nchi hiyo, Sheikh Isa Qassim.
-
Al Wifaq yasisitiza kuachiwa huru wanawake wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa Aal Khalifa
Apr 12, 2018 02:47Jumuiya ya Kiislamu ya al Wifaq ya nchini Bahrain imetaka kuachiwa huru wanawake waliofungwa katika jela za utawala wa Aal Khalifa ambao walitiwa mbaroni kwa sababu tu ya kuwasilisha maoni na fikra zao.
-
Kulaaniwa wimbi jipya la kamatakamata nchini Bahrain
Apr 11, 2018 00:03Kituo cha Haki za Binadamu cha Bahrain kimetoa taarifa maalumu inayoeleza juu ya kutiwa mbaroni na vikosi vya usalama vya utawala wa Aa Khalifa wapinzani 21 na kulaani vikali hatua hiyo.
-
Vikosi vya usalama Bahrain vyawashambulia waandamanaji
Apr 07, 2018 03:24Maafisa usalama wa Bahrain wamewashambulia wananchi waliokuwa wamemininika mabarabarani kushiriki maandamano ya kupinga kufanyika nchini humo mashindano ya magari ya Langalanga maarufu kama Formula 1.
-
Matokeo ya kufunguliwa kituo cha kijeshi cha Uingereza nchini Bahrain
Apr 06, 2018 23:52Uingereza imefungua kituo chake cha kwanza cha kudumu cha kijeshi katika eneo la Ghuba ya Uajemi huko katika Bandari ya Salman nchini Bahrain.