Al Wifaq yasisitiza kuachiwa huru wanawake wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa Aal Khalifa
(last modified Thu, 12 Apr 2018 07:17:05 GMT )
Apr 12, 2018 07:17 UTC
  • Al Wifaq yasisitiza kuachiwa huru wanawake wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa Aal Khalifa

Jumuiya ya Kiislamu ya al Wifaq ya nchini Bahrain imetaka kuachiwa huru wanawake waliofungwa katika jela za utawala wa Aal Khalifa ambao walitiwa mbaroni kwa sababu tu ya kuwasilisha maoni na fikra zao.

Jumuiya hiyo ya nchini Bahrain jana ilitoa taarifa na kutangaza kuwa kuwaweka chini ya mashinikizo wanawake wa Bahrain ni siasa rasmi zinazotekelezwa na utawala wa Aal Khalifa kwa lengo la kuzima harakati kubwa ya kitaifa nchini humo inayodai uadilifu, kutekelezwa demokrasia na kuasisiwa serikali itakayochaguliwa na wananchi. 

Katika taarifa yake hiyo, Jumuiya ya Kiislamu ya al Wifaq imeashiria kutiwa mbaroni na kuteswa mamia ya wanawake wa Bahrain katika miaka kadhaa iliyopita kwa tuhuma za uwongo na kueleza kuwa utawala wa Aal Khalifa unawahoji na kuwatia mbaroni waume na watoto wa wanawake hao ikiwa ni radiamali yake kwa maandamano ya amani yanayofanywa na wanawake hao wa Bahrain sambamba na kuwaweka chini ya mashinikizo wapinzani nchini humo. 

Maandamano ya amani ya wanawake nchini Bahrain

Muundo wa kisiasa uliopo nchini Bahrain ni tatizo kuu na la kimsingi zaidi ambalo limekuwa likiibua upinzani wa wananchi dhidi ya utawala wa Aal Khalifa; muundo ambao umeasisiwa kwa misingi ya udikteta na ukandamizaji. Nchi hiyo ilianza kushuhudia mapinduzi ya wananchi dhidi ya utawala huo ulioko madarakani wa Aal Khalifa tangu Februari 14 mwaka 2011 huku ukandamizaji unaofanywa na utawala huo ukizitia hofu na wasiwasi fikra za waliowengi na taasisi za kutetea haki za binadamu.

Tags