UN: Maisha ya maelfu ya wanawake Gaza yako hatarini huku Israel ikiendeleza vita
(last modified 2024-10-08T03:02:09+00:00 )
Oct 08, 2024 03:02 UTC
  • UN: Maisha ya maelfu ya wanawake Gaza yako hatarini huku Israel ikiendeleza vita

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kazi ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake linasema maelfu ya wanawake wanakabiliwa na hatari za kiafya zinazohatarisha maisha katika Ukanda wa Gaza, ambapo zaidi ya Wapalestina 42,000 wameuawa kutokana na vita vya mauaji ya kimbari vinavyowendelezwa na utawala katili wa Israel.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linalojulikana kama UN Women lilisema katika ripoti yake siku ya Jumapili kuwa zaidi ya asilimia 85 ya vituo vya afya katika eneo hilo la pwani vimeharibiwa, na hivyo kuvuruga huduma za matibabu na kuwapa changamoto wanawake kupata huduma muhimu za afya.

Ripoti hiyo pia imesisitiza haja ya kukidhi mahitaji ya dharura kwa wanawake na washichama wa Gaza, kama vile matibabu ya saratani, huduma za afya ya uzazi, na msaada wa kisaikolojia.

Israel ilianzisha mashambulizi yake ya mauaji ya  kimbari ya Gaza mnamo Oktoba 7, 2023, baada ya Hamas kutekeleza operesheni ya kihistoria dhidi ya utawala huo katilia ili kulipiza kisasi dhulma zinazozidi kufanywa na utawala huo dhidi ya watu wa Palestina.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, Utawala wa Israel hadi sasa umewaua Wapalestina wasiopungua 42,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kujeruhi wengine 97,303.

Israel pia imekuwa ikilenga kwa makusudi shule, misikiti na hospitali za eneo lote la Gaza ambalo ambalo imelizingira.

Tags