-
Dosari zagubika kura ya maoni ya marekebisho ya Katiba Burundi (SAUTI)
May 17, 2018 10:24Wananchi wa Burundi waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wameshiriki katika kura ya maoni ya marekebisho ya Katiba ambayo kama itapasishwa itamfungulia njia Rais Pierre Nkurunziza kuiongoza nchi hiyo hadi 2034.
-
SAUTI, Miili ya watu 26 waliouawa hivi karibuni Burundi imezikwa, huku Bujumbura ikituma ujumbe kwa DRC
May 15, 2018 12:10Hatimaye miili ya watu 26 waliouawa hivi karibuni nchini Burundi na kundi la watu wasiojulikana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imezikwa leo, katika mazishi yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi hiyo.
-
SAUTI, Kampeni ya uchaguzi wa kura ya maoni nchini Burundi imefungasha virago jioni ya leo katika anga ya mchuano mkali
May 14, 2018 12:34Kampeni ya wiki mbili ya uchaguzi wa kura ya maoni nchini Burundi imekamilisha shughuli zake jioni ya (leo) Jumatatu ambapo vyama vya kisiasa vilipata wasaa wa kuwafikishia maoni yao wananchi.
-
SAUTI, Jeshi la Burundi lasema, watu waliotekeleza shambulizi jana na kuua watu 26 wasifurahie kwani watapatikana
May 12, 2018 12:18Watu 26 wameuawa nchini Burundi na wengine saba kujeruhiwa kufuatia shambulio la watu wasiojulikana kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
-
Taharuki Burundi, maafisa wa serikali wataka 'kuhasiwa maadui'
May 08, 2018 12:31Huku zikiwa zimesalia chini ya wiki mbili kabla ya wananchi wa Burundi kushiriki kwenye kura ya maoni ya kuifanyia marekebisho katiba ya nchi, hali ya taharuki imetanda nchini humo huku maafisa wa serikali wakitoa mwito wa kushambuliwa watu wanaopinga kufanyika kwa zoezi hilo.
-
Wiki mbili kabla ya kufanyika kura ya maoni, Burundi yazipiga marufuku BBC na VOA
May 05, 2018 10:27Serikali ya Burundi imeyapiga marufuku mashirika ya utangazaji ya BBC na VOA pamoja na stesheni mbili za habari za ndani kuendesha shughuli zao nchini humo zikiwa zimesalia takriban wiki mbili kabla ya kufanyika kura ya maoni ya mabadiliko ya katiba.
-
Kanisa Katoliki nchini Burundi lapinga kura ya maoni
May 04, 2018 02:53Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Burundi wamepinga kura ya maoni ya kuifanyia marekebisho katiba ya nchi inayotazamiwa kufanyika mwezi huu.
-
SAUTI, Chama tawala cha CNDD-FDD nchini Burundi, chafungua pazia la kampeni ya uchaguzi wa kura ya maoni
May 03, 2018 11:46Kampeni ya kutetea kura ya 'ndio' ama 'hapana' kwa ajili ya kura ya maoni nchini Burundi na ambayo itaruhusu marekebisho ya katiba nchini humo, tayari imefunguliwa rasmi.
-
Rais Pierre Nkurunziza alifanyia marekebisho baraza lake la mawaziri Burundi
Apr 20, 2018 09:47Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
-
HRW: Maafisa usalama na chama tawala wanaua wapinzani Burundi
Apr 17, 2018 23:35Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema maafisa usalama wakishirikiana na wafuasi wa chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD wanawaua na kuwashambulia wapinzani hususan wanaoonekana kupinga kura ya maoni inayotazamiwa kufanyika mwezi ujao.