Dosari zagubika kura ya maoni ya marekebisho ya Katiba Burundi (SAUTI)
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i44622-dosari_zagubika_kura_ya_maoni_ya_marekebisho_ya_katiba_burundi_(sauti)
Wananchi wa Burundi waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wameshiriki katika kura ya maoni ya marekebisho ya Katiba ambayo kama itapasishwa itamfungulia njia Rais Pierre Nkurunziza kuiongoza nchi hiyo hadi 2034.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
May 17, 2018 10:24 UTC

Wananchi wa Burundi waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wameshiriki katika kura ya maoni ya marekebisho ya Katiba ambayo kama itapasishwa itamfungulia njia Rais Pierre Nkurunziza kuiongoza nchi hiyo hadi 2034.

Kura ya maoni imefanyika nchini Burundi huku dosari kadha wa kadha zikishuhudiwa. Aidha mmoja wa waangalizi wa muungano wa upinzani amekamatwa. Hata hivyo kwa jumla upigaji kura umefanyika salama salmin zoezi ambalo limepongezwa na Rais Pierre Nkurunziza.

Mwandishi wetu wa Bujumbura, Hamida Issa ana maelezo zaidi……