-
Kiongozi Muadhamu: Kuhitimishwa satwa ya Daesh ni pigo kwa Marekani na tawala tegemezi kwa Washington
Nov 22, 2017 08:07Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kuhitimishwa satwa ya mti khabithi wa kundi la kigaidi la Daesh ni pigo kwa serikali za huko nyuma na za sasa za Marekani pamoja na tawala vibaraka na tegemezi kwa Washington katika Mashariki ya Kati ambazo zililianzisha kundi hili na kuliunga mkono kwa hali na mali ili zitanue satwa zao katika eneo hili na hivyo kuufanya utawala ghasibu wa Israel uwe na udhibiti wa eneo hili.
-
Rais Rouhani: Kushindwa magaidi wa Daesh ni habari njema kwa Iran na Mashariki ya Kati
Nov 21, 2017 14:22Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kung'olewa mizizi ya kundi la kigaidi la Daesh na kusambaratishwa misingi yake huko nchini Syria ni habari njema kwa wananchi wa Iran na wa mataifa ya Mashariki ya Kati.
-
Hizbullah: Marekani imeisadia Daesh huko al Bukamal
Nov 21, 2017 03:39Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Marekani imeilisaidia kundi la kigaidi la Daesh katika mapigano ya hivi majuzi katika mji wa al Bukamal nchini Syria hatua ambayo inakadhibisha madai ya Washington kwamba inapambana na ugaidi
-
Kusambaratishwa kikamilifu DAESH (ISIS) nchini Iraq
Nov 19, 2017 07:30Mabadiliko yanayojiri kwenye medani za vita nchini Iraq yanabainisha kusambaratishwa na kutokomezwa Daesh (ISIS) nchini humo; na kushindwa kikamilifu kundi hilo la kigaidi na kitakfiri ambako ni sawa na kupata mafanikio makubwa Wairaqi katika mapambano dhidi ya magaidi kumeakisiwa sana na duru mbalimbali za habari.
-
Mamia ya viwiliwili vya magaidi wa ISIS vimehifadhiwa katika vyumba vya maiti Libya
Nov 14, 2017 07:26Libya imetangaza habari ya kuhifadhiwa mamia ya viwiliwili vya magaidi wa Daesh katika mji wa Misrata tangu mwaka mmoja uliopita.
-
Marekani yaua raia 16 kwa niaba ya ISIS mashariki mwa Syria
Nov 13, 2017 04:17Kwa akali raia 16 wameuawa katika mashambulizi mapya ya anga yaliyofanywa na ndege za kivita za Marekani mashariki mwa Syria, siku chache baada ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) kutimuliwa katika eneo hilo.
-
Karzai: Marekani inashirikiana na ISIS (Daesh) nchini Afghanistan
Nov 12, 2017 13:41Rais wa zamani wa Afghanistan, Hamid Karzai amesema Marekani inafanya kazi bega kwa bega na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika nchi hiyo inayoshuhudia vita na ukosefu wa uthabiti kwa miaka mingi sasa.
-
Kusambaratishwa ISIS mashariki mwa Syria
Nov 10, 2017 02:34Hatua ya wanajeshi wa Syria na waitifaki wao ya kuingia katika mji wa mpakani wa al-Bukamal ina maana ya kusambaratishwa kikamilifu magaidi wa Daesh (ISIS) mashariki mwa nchi hiyo. Mafanikio hayo makubwa yaliyopatikana katika vita dhidi ya ugaidi yamekuja wiki moja baada ya kukombolewa mji wa kiistratijia wa Deir ez-Zor kutoka katika makucha ya magaidi wa ISIS wanaoungwa mkono na madola ya kigeni ukiwemo utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Iran: Hujumu dhidi ya wakimbizi Syria, ishara ya kusambaratika ISIS Deir Ezzor
Nov 05, 2017 14:53Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali shambulizi la bomu dhidi ya mkusanyiko wa wakimbizi katika mji wa Deir Ezzor, mashariki mwa Syria, lililosababisha vifo vya makumi ya watu.
-
Hizbullah ya Iraq: Baada ya Daesh kushindwa, Marekani na Israel zinapanga njama mpya
Nov 02, 2017 17:20Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu 'Kataib Hizbullah' nchini Iraq sambamba na kutangaza kuwa, genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh lilikuwa na mpango wa uharibifu kupitia ajenda za Marekani, Israel na fedha za baadhi ya nchi za Kiarabu, imesema kuwa baada ya kumalizika vita dhidi ya kundi hilo Iraq inatakiwa kujiweka tayari kwa ajili ya njama mpya za Washington na washirika wake.