Marekani yaua raia 16 kwa niaba ya ISIS mashariki mwa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i36357-marekani_yaua_raia_16_kwa_niaba_ya_isis_mashariki_mwa_syria
Kwa akali raia 16 wameuawa katika mashambulizi mapya ya anga yaliyofanywa na ndege za kivita za Marekani mashariki mwa Syria, siku chache baada ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) kutimuliwa katika eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 13, 2017 00:47 UTC
  • Marekani yaua raia 16 kwa niaba ya ISIS mashariki mwa Syria

Kwa akali raia 16 wameuawa katika mashambulizi mapya ya anga yaliyofanywa na ndege za kivita za Marekani mashariki mwa Syria, siku chache baada ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) kutimuliwa katika eneo hilo.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limeripoti kuwa, raia wasiopungua 10 wameuawa katika hujuma za anga za muungano wa kijeshi wa Marekani katika kijiji cha al-Duwaiji, wilaya ya Tal Shaer katika mkoa wa Deir Ezzor ulioko mpakani mwa nchi hiyo na Iraq.

Habari zinasema kuwa, idadi kubwa ya madaktari wameuawa walipokuwa wakijaribu kuokoa maisha ya watu waliokuwa wamefukiwa kwenye vifusi vya majengo yaliyolengwa na mashambulizi hayo ya anga ya Marekani.

Kadhalika raia wengine sita wameuawa katika shambulizi tofauti la US, dhidi ya kijiji cha al-Da’ij, katika mkoa wa Hasakah. 

Ndege za kijeshi za Marekani katika anga ya Syria

Mapema mwezi huu, jeshi la Syria lilitangaza habari ya kufanikiwa kuchukua udhibiti kamili wa mji wa Deir Ezzor ulioko mashariki mwa nchi na kuwatimua kabisa magaidi wakufurishaji wa ISIS waliouteka mji huo wa kistratajia mwaka 2014.

Weledi wa mambo wanasema hatua ya Marekani kushambulia makazi ya raia katika mji huo muhimu inalenga kuwapa moyo na kuwashajiisha wanachama wa Daesh, waliotimuliwa mjini hapo Novemba 3.