Hizbullah: Marekani imeisadia Daesh huko al Bukamal
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i36585-hizbullah_marekani_imeisadia_daesh_huko_al_bukamal
Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Marekani imeilisaidia kundi la kigaidi la Daesh katika mapigano ya hivi majuzi katika mji wa al Bukamal nchini Syria hatua ambayo inakadhibisha madai ya Washington kwamba inapambana na ugaidi
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Nov 21, 2017 00:09 UTC
  • Hizbullah: Marekani imeisadia Daesh huko al Bukamal

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Marekani imeilisaidia kundi la kigaidi la Daesh katika mapigano ya hivi majuzi katika mji wa al Bukamal nchini Syria hatua ambayo inakadhibisha madai ya Washington kwamba inapambana na ugaidi

Sayyid Hassan Nasrullah ambaye alikuwa akizungumzia ushindi wa Syria na waitifaki wake na kuangamizwa kundi la kigaidi la Daesh katika mji huo amesema kuwa, kukombolewa kwa mji wa al Bukamal ambao ulikuwa wa mwisho kutwaliwa na wapiganaji wa kundi la Daesh nchini Syria ni ushindi mkubwa.

Amesema kuwa Marekani imelisaidia kundi la Daesh katika mapigano ya Bukamal kadiri ilivyoweza na kwamba iliwasaidia wapiganaji wa kundi hilo kwa kuwapa kivuniko cha anga, kuwapa taarifa za kiintelijensia na kiupelelezi juu ya maeneo ya jeshi la Syria, wapiganaji wa Hizbullah na washirika wao, kusimamia vita vya kielektroniki na kadhalika.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameongeza kuwa, Marekani pia iliwasafirisha kwa helikopta makamanda wa kundi la kigaidi na Kiwahabi la Daesh baada ya kipigo cha al Bukamal na kuwapeleka katika maeneo yanayodhibitiwa na wapinzani wa serikali ya Damascus.

Sayyid Hassan Nasrullah

Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa kukombolewa kwa Bukamal kuna maana ya kumalizika kabisa Daesh kama kundi la kijeshi na eti dola la Khilafa katika chini za Iraq na Syria lakini ametahadharisha kuwa wapiganaji wa kundi hilo wangalipo huku na kule katika maeneo mbalimbali ya Syria.

Sayyid Nasrullah amesema ushindi dhidi ya kundi la Daesh ni ushindi wa maadili na thamani za Kiislamu dhidi ya ukatili na unyama wa magaidi wa Kiwahabi wanaoungwa mkono na Saudi Arabia na Marekani.

Jeshi la Syria, wapiganaji wa Hizbullah na washirika wao walifanikiwa kuukomboa mji wa al Bukamal ulioko kwenye mpaka wa nchi hiyo na Iraq kutoka kwenye makucha machafu ya kundi la Kiwahabi la Daesh Jumapili iliyopita.