-
Rais Rouhani: Daesh na waungaji mkono wa ugaidi, ni dhihirisho la fikra mgando na unafiki wa zama hizi
Aug 18, 2017 04:13Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kwamba, genge la Daesh (ISIS) na waungaji mkono wa ugaidi, ni dhihirisho la fikra mgando na unafiki uliochupa mpaka katika zama hizi.
-
Meja Jenerali Jaafari: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni chimbuko la heshima izza ulimwenguni
Aug 14, 2017 03:35Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, SEPAH, amesema kuwa, kuwa mfuasi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni fakhari kwa watu huru duniani na kwamba, mapinduzi haya ni chimbuko la izza na heshima ulimwenguni.
-
Polisi wanne wa Misri wauawa katika shambulizi la Daesh eneo la Sinai
Aug 10, 2017 14:42Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daeh (ISIS) limekiri kutekeleza shambulizi dhidi ya gari la polisi ya Misri na kuua maafisa wanne wa usalama katika eneo la Sinai.
-
Kissinger: Kuwepo Daesh (ISIS) ni muhimu kwa ajili ya kuidhibiti Iran
Aug 10, 2017 03:44Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani Henry Kissinger ameonya kuwa serikali ya Washington itafanya makosa kuliangamiza kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) kwa sababu kuwepo kwake ni muhimu kwa ajili ya kuidhibiti Iran.
-
Iran yawatia mbaroni makumi ya magaidi wa Daesh/ISIS
Aug 08, 2017 07:51Vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimewakamata wanachama 27 wenye mfungamano na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) waliokuwa wanapanga njama ya kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini.
-
Ndege za kivita za Marekani zauwa raia 18 Syria
Aug 04, 2017 08:10Ndege za kivita za muungano unaoongozwa na Marekani kwa mara nyingine tena zimeua raia 18 katika mji wa Raqqah kaskazini mwa Syria.
-
UN yaipongeza al Hashdu sh-Sha'abi kwa mapambano yake dhidi ya Daesh
Aug 02, 2017 02:51Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Iraq amepongeza nafasi ya harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi katika kufanikisha ukombozi wa miji mbalimbali ya Iraq na kulinda maisha ya raia katika vita dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh.
-
Mke wa mufti wa Daesh Tal Afar ajiua na watoto wake watatu
Jul 31, 2017 15:36Duru za kuaminika nchini Iraq zimeripoti kuwa, mke wa mufti wa kundi la Daesh amejiua yeye na watoto wake watatu katika mji wa Tel Afar huko kaskazini mwa Iraq.
-
Waingereza 150 wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh wavuliwa uraia
Jul 30, 2017 15:13Serikali ya Uingereza imewavua uraia zaidi ya raia wake 150 kwa tuhuma za kujiunga na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS).
-
Raia 29 wauawa katika jinai mpya za muungano unaoongozwa na Marekani nchini Syria
Jul 27, 2017 08:04Raia 29 wa Syria jana waliuawa katika mashambulizi ya ndege za kivita za muungano eti wa kimataifa wa kupambana na Daesh unaoongozwa na Marekani. Mashambulizi hayo yalifanywa katika mji wa Raqqah kaskazini mwa Syria.