Waingereza 150 wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh wavuliwa uraia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i32472-waingereza_150_wanachama_wa_kundi_la_kigaidi_la_daesh_wavuliwa_uraia
Serikali ya Uingereza imewavua uraia zaidi ya raia wake 150 kwa tuhuma za kujiunga na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS).
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 30, 2017 15:13 UTC
  • Waingereza 150 wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh wavuliwa uraia

Serikali ya Uingereza imewavua uraia zaidi ya raia wake 150 kwa tuhuma za kujiunga na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS).

Gazeti la Times limeandika kuwa uraia wa raia zaidi ya 150 wa nchi hiyo umefutwa kwa tuhuma za watu hao kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh na kwamba wamezuiliwa pia kurejea nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti hilo, raia hao wa Uingereza waliojiunga na Daesh hivi sasa wako nje ya nchi.

Baada ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh kushindwa vibaya katika nchi za Syria na Iraq kurejea katika nchi za Ulaya raia wa nchi hizo wanachama wa kundi hilo kumewatia wasiwasi mkubwa viongozi wa nchi hizo wakiwemo wa Uingereza.

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa serikali ya Uingereza, watu 850 raia wa nchi hiyo wamesafiri kuelekea Syria kujiunga na makundi ya kigaidi ambapo hadi sasa 130 kati yao wameuawa lakini nusu yao wamesharejea nchini Uingereza.

Magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh

Maafisa wa usalama wa Uingereza vilevile wametoa indhari kuhusu kurejea nchini humo Waingereza wengine 300 wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.

Viongozi wa serikali ya London wanaeleza kutiwa wasiwasi na kurejea nchini humo raia wao waliojiunga na kundi la kigaidi la Daesh katika hali ambayo, Marekani na serikali kadhaa za nchi za Magharibi waitifaki wa Washington ni waungaji mkono wakuu wa makundi ya kigaidi.../