Iran: Utawala wa kizayuni hauna mpaka katika kutenda jinai
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i133518-iran_utawala_wa_kizayuni_hauna_mpaka_katika_kutenda_jinai
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, utawala haramu wa Israel hauna mpaka katika kutenda jinai na wqala hauheshimu ahadi wala sheria yoyote ya kimataifa.
(last modified 2025-11-23T14:50:00+00:00 )
Nov 23, 2025 14:49 UTC
  • Iran: Utawala wa kizayuni hauna mpaka katika kutenda jinai
    Iran: Utawala wa kizayuni hauna mpaka katika kutenda jinai

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, utawala haramu wa Israel hauna mpaka katika kutenda jinai na wqala hauheshimu ahadi wala sheria yoyote ya kimataifa.

Ismail Baghaei amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari leo ambapo ameashiria jinai za utawala huo ghasibu katika Ukanda wa Gaza na kusema kuwa, Wapalestina 24 wasio na hatia waliuawa shahidi katika ukanda huo siku ya Jumamosi ya jana pekee.

Msemaji Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha ameashiria habari iliyochapishwa kuhusu utawala wa Kizayuni kutumia silaha zilizopigwa marufuku yakiwemo mabomu ya vishada kusini mwa Lebanon na pia wizi wa viungo vya miili ya wafungwa wa Kipalestina unaofanywa na utawala huo na kuongeza kuwa: "matukio hayo yanazzidi kuthibitiisha kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel hauna mipaka yoyote na wala hauheshimu sheria katika kutekeleza jinai zake."

Kadhalika Ismail Baghaei amesema, Marekani haiko makini kuhusu kufanya mazungumzo, na kuongeza: "utendaji wa Washington umezuia  kufanyika mazungumzo ya maana."

Katika radiamali yake kuhusiana na kupasishwa azimio dhidi ya Iran na nchi tatu za Ulaya na Marekani katika Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki amesema: "Azimio hili litalitatiza suala hilo badala ya kusaidia kulitatua."