Rais Erdogan: Amani haiwezi kupatikana pasi na kuundwa taifa la Palestina
-
Erdogan: Amani haiwezi kupatikana bila kuundwa taifa la Palestina
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kuwa, amani haiwezi kupatikana bila kuundwa taifa la Palestina.
Akitangaza mashauriano na mwenzake wa Russia kuhusiana na jinai za Wazayuni Rais wa Uturuki amesema: "amani haiwezi kupatikana bila ya kuasisiwa taifa la Palestina."
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa, himaya na uungaji mkono usioyumba wa Afrika Kusini kwa kadhia ya Palestina ni wa thamani sana; Afrika Kusini ilichukua msimamo wa kijasiri wakati wa mauaji ya kimbari ya Gaza, ambapo Wapalestina 70,000 waliuawa shahidi.
Ninaipongeza Afrika Kusini kwa msimamo wake wa kijasiri wa kufungua kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).
Afrika Kusini iliwasilisha kesi hiyo mwezi Disemba 2023 ikiituhumu Israel kwa mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza. Tangu wakati huo, mataifa kadhaa yamejiunga na mchakato huo wa kisheria.