-
Katibu Mkuu wa UN ahimiza mwenendo wa kukomeshwa satua ya Marekani duniani
Sep 14, 2018 09:49Tangu Donald Trump aliposhika hatamu za kuiongoza Marekani amekuwa akitekeleza siasa za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja kuhusiana na masuala ya kimataifa. Ikulu ya Rais wa Marekani,White House, tofauti kabisa na uhakika wa mambo, inadai kwamba siasa za Trump zimeipa tena Marekani usukani wa kuiongoza dunia, madai ambayo yamewashangaza wachambuzi na weledi wa mambo.
-
Donald Trump amevunja rekodi ya kusema uongo
Sep 13, 2018 23:01Gazeti maarufu la Washington Post la nchini Marekani limesema kuwa, rais wa nchi hiyo Donald Trump amevunja rekodi zote za kusema uongo.
-
Yemen: Trump na washirika wake wanahusika na mauaji al Hudaydah
Sep 13, 2018 09:25Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amesema kuwa Rais Donald Trump wa Marekani, Saudi Arabia na Imarati wanahusika na mauaji ya wakazi wa mji wa al Hudaydah.
-
Utafiti: Wapalestina wengi hawana imani na Trump
Sep 12, 2018 09:21Utafiti mpya uliofanywa na Kituo cha Utafiti na Sera cha Palestina umeonesha kuwa, aghalabu ya Wapalestina hawana imani na Rais Donald Trump wa Marekani na wala hawataki serikali ya Washington ijihusishe na mazungumzo ya amani ya nchi yao.
-
Trump kuwafukuza Wapalestina nchini Marekani
Sep 10, 2018 02:54Gazeti moja la nchini Marekani limeripoti kuwa, mshauri wa usalama wa taifa wa White House, leo Jumatatu atatangaza kufungwa ofisi ya Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO mjini Washington.
-
Davenport: Baraza la Usalama limsaili Trump kwa nini Marekani imejiondoa JCPOA
Sep 09, 2018 11:33Mkurugenzi wa Sera za Kuzuia Silaha za Maangamizi katika Shirika la Kudhibiti Silaha la Marekani amewataka wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamuweke kiti moto Rais Donald Trump wa Marekani wakati atakapohudhuria kikao cha baraza hilo.
-
Kiongozi wa Upinzani Afrika Kusini asema Kenya ni koloni la Marekani, akipigia chapuo Kiswahili
Aug 31, 2018 02:28Kiongozi maarufu wa upinzani nchini Afrika Kusini amekosoa vikali safari ya hivi karibuni ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya nchini Marekani na mazungumzo yake na rais wa nchi hiyo, Donald Trump.
-
Uchunguzi: Trump, rais mbaya zaidi katika historia ya Marekani
Aug 28, 2018 01:36Matokeo ya uchunguzi wa maoni yanaonesha kuwa, wananchi wa Marekani wanamtambua Donald Trump kuwa ndiye rais mbaya zaidi katika historia ya nchi hiyo.
-
Wakulima Afrika Kusini: Trump! Tuache tupumue!
Aug 26, 2018 22:50Wakulima nchini Afrika Kusini wamekasirishwa na matamshi ya kichochezi ya rais wa Marekani, Donald Trump na kumtaka asijiingize katika mambo yasiyomuhusu.
-
Kuvunjwa safari ya Mike Pompeo Korea Kaskazini; nukta ya kubatilika madai ya Trump
Aug 26, 2018 22:48Katika kipindi cha utawala wake nchini Marekani, Rais Donald Trump amejaribu kufanya mabadiliko anayoyaona kuwa makubwa katika uga wa ndani na nje ya nchi hiyo ili kwa njia hiyo aweze kujidhihirisha kuwa rais anayependwa na aliyefanikiwa zaidi katika utekelezaji wa majukumu yake nchini humo.