Uchunguzi: Trump, rais mbaya zaidi katika historia ya Marekani
Matokeo ya uchunguzi wa maoni yanaonesha kuwa, wananchi wa Marekani wanamtambua Donald Trump kuwa ndiye rais mbaya zaidi katika historia ya nchi hiyo.
Ripoti iliyochapishwa na jarida la kila wiki la Newsweek inasema matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi za YouGov na The Economist yanaonesha kuwa asilimia 41 ya wananchi wa Marekani wanaamimi kuwa Donald Trump ndiye rais mbaya zaidi katika historia ya nchi hiyo. Matokeo hayo yanasema asilimia 28 tu ya Wamarekani wamemchagua Barack Obama kama rais mbaya zaidi katika historia ya Marekani.
Uchunguzi huo wa maoni ya Wamarekani ulifanyika katika siku za tarehe 19 hadi 21 Agosti mwaka huu wa 2018.
Matokeo ya uchunguzi huu na mwingine wa kabla yake unaonesha kuwa, Wamarekani wengi hawaridhishwi na utendaji wa Donald Trump.
Itakumbukwa kuwa katika siku za hivi karibuni Donald Trump aliutaja uchunguzi huo unaofanywa na taasisi zenye hadhi na za kitaalamu nchini Marekani kuwa ni bandia na kudai kuwa anapendwa na Wamarekani wengi.