-
Wananchi wa Mauritania waandamana kumlaani Donald Trump
Dec 11, 2017 11:02Wananchi wa Mauritania wameungana na Waislamu na wapenda haki katika kona zote za dunia kuendeleza maandamano ya kumlaani rais wa Marekani, Donald Trump kwa hatua yake ya kuitambua Quds kuwa mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.
-
Watawala vibaraka wa Kiarabu wabanwa; wananchi wataka viongozi wapya
Dec 11, 2017 09:39Malalamiko na maandamano ya wananchi wa nchi za Kiarabu si tu kwamba yamewalenga Rais Donald Trump wa Marekani na Benjamin Netanyahi, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel pekee bali pia watawala vibaraka wa Kiarabu wanafanya eti mapatano ya amani na Wazayuni kwa madhara ya ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu.
-
Somalia yasema hatua ya Trump dhidi ya Quds ni 'hatari'
Dec 10, 2017 00:10Somalia imejiunga na nchi nyingine za Afrika kulaani hatua ya Rais wa Marekani, Donald Trump ya kuitangaza Baytul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Mkuu wa Wakristo wa Misri akataa kuonana na Naibu wa Trump
Dec 09, 2017 23:25Mkuu wa Wakristo wa Qibti nchini Misri amekataa kuonana na Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence, kutokana na Donald Trump kuitangaza Baytul Muqaddas kuwa eti ni mji mkuu wa Israel.
-
Njia za kukabiliana na misimamo ya kichokozi ya Donald Trump kuhusu Quds
Dec 09, 2017 23:24Mbali na katika kona mbalimbali za dunia, maandamano makubwa ya Wapalestina na fikra za walio wengi katika ulimwengu wa Kiislamu zinaendelea kumuandama rais wa Marekani, Donald Trump kutokana na chokochoko zake za kuitangaza Baytul Muqaddas kuwa eti ni mji mkuu wa Israel.
-
Viongozi wa Kiislamu Kenya walaani hatua ya Trump dhidi ya Quds
Dec 08, 2017 23:24Viongozi wa Kiislamu nchini Kenya wamelaani uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuutangaza mji wa Baitul Muqaddas wa Palestina kuwa mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.
-
Wairani waandamana kulaani uamuzi wa Rais Trump kuhusu Baitul Muqaddas
Dec 08, 2017 11:29Maelfu ya wananchi wa Iran wameandamana leo baada ya Swala ya Ijumaa katika miji mbalimbali hapa nchini wakilalamikia na kulaani uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuutambua mji wa Baitul Muqaddas wa Palestina kama mji mkuu wa utawala vamizi wa Israel.
-
Matokeo ya uamuzi wa Trump kuhusu Quds kwa usalama wa Mashariki ya Kati
Dec 08, 2017 04:16Uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kutambua rasmi Quds Tukufu kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel na wakati huohuo kuamuru kuhamishiwa huko ubalozi wa Marekani kutoka mjini Tel Aviv bila shaka utakuwa na matokeo muhimu kwa eneo zima la Mashariki ya Kati.
-
Radiamali ya Umoja wa Ulaya kuhusu hatua ya Trump dhidi ya Quds Tukufu
Dec 08, 2017 01:18Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amelaani hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kutambua rasmi mji wa Beitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel na kuongeza kuwa hatua hiyo ya upande mmoja bila shaka itavuruga utulivu wa ulimwengu na juhudi zote zilizofanywa kwa ajili ya kutatua mzozo wa Palestina.
-
Iran yatoa jibu kwa uamuzi wa Marekani wa kuhamishia ubalozi wake Baitul Muqaddas
Dec 07, 2017 00:36Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa maalumu, ambayo mbali na kulaani kutangazwa Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israel imesisitiza pia kwamba tangazo hilo lilotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani ni ukiukaji wa wazi wa maazimio ya kimataifa.