-
Ubelgiji yalilaumu vikali Baraza la Usalama kwa kushindwa kulinda misingi ya Hati ya UN
Feb 26, 2025 11:38Naibu waziri mkuu wa Ubelgiji Maxime Prevot amesema "amesikitishwa sana" kuona Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kutuma ujumbe wazi wa kuunga mkono sheria za kimataifa, na akatoa wito wa kuchukuliwa hatua kali zaidi za kimataifa za kulinda haki za binadamu na kuwawajibisha wakiukaji wa sheria.
-
Shirika la DAWN lataka ICC imchunguze Rais wa Marekani
Feb 25, 2025 02:57Shirika moja lisilo la serikali limeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuanzisha uchunguzi dhidi ya Rais Donald Trump wa Marekani, kutokana na mienendo yake dhidi ya maafisa wa korti hiyo ya kimataifa iliyoko The Hague huko Uholanzi.
-
Madai yasiyo na msingi ya Trump na sisitizo lake la kuendeleza sera ya mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran
Feb 22, 2025 02:30Akirejelea siasa zake za mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Donald Trump wa Marekani kwa mara nyingine tena amedai kuwa, siasa hizo zinalenga kuleta amani na kwamba Washington haitairuhusu Iran na nchi nyingine kupata silaha za nyuklia.
-
Trump asisitiza tena kuigeuza Canada jimbo la 51 na kuzipora Greenland na Mfereji wa Panama
Feb 21, 2025 10:47Rais Donald Trump wa Marekani amesisitiza tena juu ya nia yake ya kuiunganisha Canada na Marekani na kuifanya jimbo la 51 la nchi hiyo, pamoja na azma yake ya kulinyakua eneo la Greenland na Mfereji wa Panama.
-
EU yamkingia kifua Zelensky baada ya kushambuliwa vikali na Trump
Feb 21, 2025 06:50Mvutano kati ya Ulaya na Marekani umeendelea kushtadi, baada ya viongozi wa nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya kumkingia kifua Rais Vladimir Zelensky wa Ukraine, aliyeshambulia kwa maneno makali na Rais Donald Trump wa Marekani hivi karibuni.
-
Kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina; Jinai mpya dhidi ya Wapalestina
Feb 20, 2025 08:10Leo tutaangazia jinai mpya ya Wazayuni na washirika wao ya kutaka kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina katika makazi na nchi yao.....
-
Jeshi la Sudan lasonga mbele katika mji mkuu Khartoum na mji wa Bahri
Feb 18, 2025 13:41Jeshi la Sudan limetangaza kuwa linaendelea kusonga mbele katika mji mkuu Khartoum na mji wa Bahri ulioko kaskazini mwake, na kutwaa udhibiti wa vitongoji kadhaa.
-
Msomi wa Misri amshambulia vikali Trump, aitaka Cairo kusimama kidete dhidi ya bwabwaja zake
Feb 13, 2025 06:51Msomi wa Misri amemshambulia vikali Rais Donald Trump wa Marekani na kutoa wito wa kutolewa jibu kali dhidi ya kiongozi huyo akisema: "Lazima tusimame imara na ngangari dhidi ya Trump, na misaada ya Marekani inapaswa kupelekwa kuzimu."
-
Mpango wa Trump kwa ajili ya Gaza; njama za kuifuta Palestina
Feb 12, 2025 06:40Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria upinzani mkubwa wa nchi za eneo na kimataifa dhidi ya mpango haramu wa Rais wa Marekani kuhusu Gaza na kueleza kwamba, mpango huo wa kuwahamisha kwa nguvu watu wa Palestina kutoka Gaza kwa mujibu wa mpango wa kikoloni wa "kuifuta Palestina".
-
Jibu la Russia kwa vitisho vya Trump dhidi ya BRICS
Feb 11, 2025 02:44Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa taarifa kuhusiana na tishio la Rais Donald Trump wa Marekani la kutoza ushuru wa asilimia 100 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nchi za BRICS iwapo dola itafutwa katika mabadilishano ya kibiashara ya nchi hizo, na kusisitiza kuwa ushirikiano wa nchi wanachama wa BRICS unalenga kuimarisha uwezo wa kijamii, kiuchumi na kibinadamu wa nchi hizo.