-
Ukosoaji mkali wa Human Rights Watch kwa Marekani kutokana na vikwazo vyake dhidi ya Iran
Oct 30, 2019 10:10Baada ya kujitoa katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA mwezi Mei 2018 serikali ya Donald Trump ya Marekani iliirejeshea Iran vikwazo vyote vilivyokuwa vimeondolewa baada ya mapatano hayo bali hata iliongeza vikwazo vingine vingi na kujigamba kuwa imeiwekea Iran vikwazo vya kiwango cha juu kabisa ambavyo havijawahi kuwekewa nchi yoyote ile duniani.
-
Trump adai pia habari ya kuuawa mrithi wa Abubakar al-Baghdadi
Oct 30, 2019 01:07Rais Donald Trump wa Marekani ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba askari wa Kimarekani wamemuua pia mrithi wa Abubakar al-Baghdadi, kiongozi wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS).
-
Kuangamizwa al Baghdadi na njama za Marekani za kujifanya inapambana na Daesh
Oct 28, 2019 02:29Marekani pamoja na waitifaki wake wa Kiarabu na Kimagharibi ndio waliolianzisha, kulitia nguvu na kuliunga mkono kwa kila namna na hali na mali; genge la kigaidi na la ukufurishaji la Daesh (ISIS) kwa shabaha ya kuiangusha serikali halali ya Syria.
-
Madai ya upotoshaji ya Trump kwamba Asia Magharibi imestawishwa na Marekani
Oct 27, 2019 04:44Baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001 na kupitia kisingizio cha kupambana na ugaidi, Marekani ilianzisha hujuma zake dhidi ya eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) ambapo mwaka 2001 Washington iliivamia kijeshi Afghanistan, huku mwaka 2003 ikiishambulia Iraq.
-
Sisitizo la Trump la kushadidisha makali katika vikwazo vya mafuta dhidi ya Iran
Oct 26, 2019 08:32Vikwazo vya nyuklia dhidi ya Iran vilitekelezwa katika marhala mbili yaani mwezi Agosti na Novemba mwaka jana baada ya Trump kutangaza kabla yake mnamo tarehe 8 Mei kuitoa Marekani katika makubaliano hayo ya nyuklia. Vikwazo hivyo vilikuwa vya upande mmoja; na vimekiuka sheria za kimataifa likiwemo azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Trump aendeleza hatua za kiuadui katika sekta ya mafuta dhidi ya Iran
Oct 26, 2019 04:49Rais Donald Trump wa Marekani ametaka zichukuliwe hatua kali zaidi za vikwazo vya mafuta dhidi ya Iran ukiwa ni muendelezo wa hatua za kiuadui na uhasama za serikali ya Washington dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Baada ya kuiita 'ng'ombe mkamwa maziwa wa Marekani', Trump aidhalilisha tena Saudia
Oct 22, 2019 23:15Rais Donald Trump wa Marekani ameidhalilisha tena Saudi Arabia na viongozi wake katika mahijiano yake na waandishi wa habari.
-
Makeke ya Trump mbele ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Oct 22, 2019 08:20Donald Trump Rais wa Marekani mwenye kubwabwaja sana tangu aingie ikulu ya White House amechukua mkondo wa sera za chuki na uhasama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na utendaji wake umejikita katika mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Tehran ili kwa njia hiyo aweze kulifanya taifa hili lisalimu amri na kukubali matakwa ya Washington.
-
Bunge la Marekani lalaani hatua ya Trump kuondoa wanajeshi wa Marekani Syria
Oct 17, 2019 23:53Hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump ya kuondoa wanajeshi wa Marekani kaskazini mwa Syria, jambo ambalo limewezesha Uturuki kushambulia eneo hilo, imekosolewa ndani ya Marekani.
-
Trump na uvamizi wa Uturuki kaskazini mwa Syria; kutoka kubariki hadi vikwazo
Oct 15, 2019 23:26Licha ya kwamba awali rais wa Marekani alibariki uvamizi wa kijeshi wa Uturuki huko kaskazini mwa Syria lakini hivi sasa amegeuka kikamilifu na kutoa amri ya kuwekewa vikwazo Ankara.