-
Trump na ahadi zake bandia za kuiondolea Iran vikwazo baada ya kufanyika mazungumzo
Sep 30, 2019 08:36Baada ya kuiondoa nchi yake kwenye mapatano ya nyuklia mwezi Mei mwaka jana na kisha kuiwekea vikwazo vikali Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika miezi ya hivi karibuni Rais Donald Trump wa Marekani ameonyesha hamu kubwa ya kutaka kufanya mazungumzo na Iran ambapo baada ya kufanya mazungumzo na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, kulienea fununu za uwezekano wa kukutana marais wa Iran na Marekani kando ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York.
-
Trump akiri: Marekani inaingilia chaguzi zinazofanyika katika nchi nyingine
Sep 28, 2019 22:57Katika kipindi cha Vita Baridi (Cold War) na baada ya vita hivyo Marekani ilikuwa ikitekeleza sera za kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine. Moja ya mambo muhimu yanayodhihirisha ukweli huo ni mienendo ya Marekani ya kuingilia chaguzi katika nchi mbalimbali kwa lengo la kuwaingiza madarakani viongozi vibaraka na wanaofuata siasa za Marekani.
-
Duru mpya ya hujuma za vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi zingine
Sep 28, 2019 04:29Marekani ina rekodi kubwa zaidi ya kutumia aina mbali mbali za vikwazo dhidi ya nchi zingine kwa ajili ya kufikia malengo ya siasa zake za nje. Ushadidishaji vikwazo unaofanywa na Washington katika kipindi cha urais wa Donald Trump umekuwa ukipingwa na kulaaniwa kimataifa. Pamoja na hayo kinachoendelea kushuhudiwa kila uchao ni kutangazwa vikwazo vingine vipya vya Marekani dhidi ya nchi zingine duniani.
-
Agizo jipya la Trump dhidi ya maafisa wa Iran na tapatapa za mfamaji
Sep 27, 2019 03:39Rais Donald Trump wa Marekani jana Alkhamisi aliendeleza sera zake za kuiweka mashinikizo ya juu zaidi kwa shabaha ya kuilazimisha Jamhuri ya Kiislamu isalimu amri mbele ya matakwa ya serikali ya Washington.
-
Maandamano dhidi ya Trump New York kabla ya mkutano wa UNGA
Sep 24, 2019 04:25Maandamano makubwa dhidi ya Rais Donald Trump wa Marekani yameshuhudiwa mjini New York usiku wa kuamkia leo, masaa machache kabla ya kuanza mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini humo.
-
Trump 'alilia' Tuzo ya Nobel, asema Obama hakustahiki kupewa
Sep 24, 2019 04:18Rais Donald Trump wa Marekani kwa mara nyingine tena amedai kuwa ana ustahiki wa kupewa Tuzo ya Amani ya Nobel.
-
Spika wa Kongresi amkosoa Trump kwa kufumbia macho jinai za utawala wa Saudia
Sep 23, 2019 03:41Bunge la Wawakilishi la Marekani, Kongresi limekemea vikali uungaji mkono na himaya ya pande zote ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo kwa utawala wa Saudi Arabia kwa kuendelea kuuzia silaha za aina mbalimbali na kutuma majeshi ya Marekani katika nchi hiyo ya kifalme kwa kisingizio cha kukabiliana na eti "vitisho".
-
Kumalizika kusikoeleweka kwa mazungumzo ya biashara kati ya Marekani na China
Sep 22, 2019 23:10Siasa za kimaslahi na za upendeleo wa kiuchumi zinazotekelezwa na Rais Donald Trump wa Marekani ambazo zinalenga kushadidisha mgogoro wa ushuru wa forodha, zimeibua vita vikubwa vya kibiashara kati ya nchi hiyo na China.
-
Trump asema uongo mara 27 katika hotuba ya dakika 95
Sep 18, 2019 20:54Televisheni ya CNN imeripoti kuwa Rais wa nchi hiyo ametoa madai ya uongo mara 27 kupitoa hotuba yake iliyochukua muda wa dakika 95.
-
Mkuu wa zamani wa Shirika la CIA akosoa udhaifu wa Trump
Sep 17, 2019 08:30Mkuu wa zamani wa Shirika la Kisasusi la Marekani (CIA), sambamba na kukosoa matamshi ya kupenda vita ya Rais Donald Trump wa Marekani, kufuatia shambulizi la ndege zisizo na rubani za Wayemen kwenye taasisi za mafuta za Saudia ARAMCO, amesema kuwa udhaifu wa kiuongozi wa rais huyo wa Marekani, umekuwa changamoto kimataifa.