Ripoti: Aghalabu ya Wamarekani hawamuamini Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57103-ripoti_aghalabu_ya_wamarekani_hawamuamini_trump
Utafiti mpya unaonesha kuwa, akthari ya wananchi wa Wamarekani wanatiwa wasiwasi na utendaji kazi wa Rais Donald Trump, na wamepoteza imani na uongozi wa mwanasiasa huyo wa chama cha Republican.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Nov 06, 2019 21:43 UTC
  • Ripoti: Aghalabu ya Wamarekani hawamuamini Trump

Utafiti mpya unaonesha kuwa, akthari ya wananchi wa Wamarekani wanatiwa wasiwasi na utendaji kazi wa Rais Donald Trump, na wamepoteza imani na uongozi wa mwanasiasa huyo wa chama cha Republican.

Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na gazeti la Washington Post kwa ushirikiano na kanali ya televisheni ya ABC yanaonesha kuwa, asilimia 58 ya Wamarekani waliotimiza masharti ya kupiga kura wanachukizwa na mtindo wa uongozi wa Trump kwa ujumla, huku asilimia 66 wakisema kuwa mwanasiasa huyo hajaendesha nchi kwa hadhi na shakhsia ya rais. 

Aidha utafiti huo unaonesha kuwa, asilimia 54 ya wananchi wa Marekani wanaamini kuwa sera ghalati za Trump zimeifanya nchi hiyo ipoteze heshima yake katika uga wa kimataifa.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, asilimia 60 ya Wamarekani wamesema kuwa Trump sio mtu wa kuaminika na mwenye muamana, hana haiba ya kuwa rais na wala haelewi changamoto na matatizo yanayowakumba wananchi wa kawaida.

Wamarekani wengi wanasema Trump ni kidhabi na mtu asiye na muamana

Takwimu na chunguzi mbalimbali za maoni zinaonyesha kuwa, Donald Trump amezidi kupoteza hali ya kuaminiwa siku baada ya siku ndani na nje ya nchi.

Septemba mwaka huu, televisheni ya CNN iliripoti kuwa Trump ametoa madai ya uongo mara 27 kupitia hotuba yake iliyochukua muda wa dakika 95.