Watetezi wa haki za binadamu: Marekani si mahala salama kwa wakimbizi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57074-watetezi_wa_haki_za_binadamu_marekani_si_mahala_salama_kwa_wakimbizi
Watetezi wa haki za binadamu wamekosoa baadhi ya sheria ngumu za uhamiaji za Marekani na kutangaza kuwa nchi hiyo si salama na mahala pa amani kwa wakimbizi katika kipindi cha utawala wa Donald Trump.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 05, 2019 12:19 UTC
  • Watetezi wa haki za binadamu: Marekani si mahala salama kwa wakimbizi

Watetezi wa haki za binadamu wamekosoa baadhi ya sheria ngumu za uhamiaji za Marekani na kutangaza kuwa nchi hiyo si salama na mahala pa amani kwa wakimbizi katika kipindi cha utawala wa Donald Trump.

Mawakili wa wakimbizi na makundi mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yalitangaza jana katika Mahakama ya Feerali ya Canada kwamba Marekani si mahala salama kwa wakimbizi na kwamba makubaliano ya nchi hizo mbili ambayo yanawalazimisha watu kwanza kuomba ukimbizi nchini Marekani yanapaswa kufutiliwa mbali. 

Mawakili wa wakimbizi waliorejeshwa Canada kutoka Marekani wametoa changamoto mahakamani kuhusiana na makubaliano hayo na kutangaza kuwa Marekani si mahala salama na eneo lenye amani kwa wakimbizi katika kipindi cha uongozi wa Trump. 

Wakimbizi wanazuiwa kuingia Marekani

Mawakili hao wameashiria idadi kubwa ya wakimbizi ambao wamefungwa jela na katika seli za mtu mmoja huko Marekani , na kuitaka Canada ichunguze hali ya Marekani kuhusiana na masuala ya usalama wa wakimbizi. 

Tangu aliposhika madaraka ya nchi, Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akitekeleza siasa za kuzuia wakimbizi kuingia nchini humo, suala ambalo limekosolewa sana na jamii ya kimataifa.