-
Makamanda wa makundi ya kigaidi nchini Syria wakimbilia upande wa jeshi la Israel
Jul 23, 2018 22:53Sambamba na jeshi la Syria kuimarisha mzingiro dhidi ya makundi ya kigaidi kusini mwa nchi hiyo, makamanda wa makundi hayo na kupitia taa ya kijani ya utawala wa Kizayuni, wamekimbilia upande wa jeshi la Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
-
Jeshi la Syria lazingira ngome ya jeshi vamizi la Marekani katika mpaka wa Iraq
Jun 22, 2018 09:37Sambamba na operesheni ya kuyasafisha maeneo mapana ya jangwa la Syria, hasa eneo la al-Badiya kutoka mikononi mwa mabaki ya wanachama wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS), jeshi la Syria limezingira ngome ya askari vamizi wa Marekani katika eneo la al-Tanf lililopo katika mpaka wa nchi hiyo na Iraq.
-
Kufichuliwa njama ya Marekani ya kuingiza tena magaidi nchini Iraq
Jun 07, 2018 02:21Matukio ya mwaka mmoja uliopita nchini Iraq ambapo magaidi wakufurishaji wa ISIS au Daesh wamesambaratishwa na kutumiliwa kikamilifu kutoka maeneo yote waliyokuwa wameyateka kufuatia jitihada za jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi, yameiandaa Iraq kuingia duru mpya ya baada ya Daesh na kuandaa mazingira ya uchaguzi wa bunge uliofanyika mwezi uliopita.
-
Syria: Kunaandaliwa mazingira ya kubuni igizo la shambulio la kemikali mashariki mwa Furat
May 30, 2018 23:12Kamisheni ya taifa nchini Syria inayoshughulikia utekelezwaji wa makubaliano ya kuzuia silaha za kemikali, imeonya juu ya kuandaliwa igizo la kubuni la shambulio la silaha hizo katika moja ya maeneo yanayodhibitiwa na wanamgambo wa Kikurdi wa 'Syrian Democratic Forces' kwa kushirikiana na askari wa Marekani, mashariki mwa mto Furat nchini humo.
-
Magaidi wakufurishaji wabomoa makaburi katika kusaka mali na dhahabu Afrin, Syria
May 25, 2018 21:51Magaidi wakufurishaji nchini Syria wamevamia makaburi ya shakhsia wa kidini na wanaoheshimiwa wa mji wa Afrin katika kusaka mali na dhahabu ndani ya makaburi hayo.
-
Jeshi la Syria lafanikiwa kudhibiti barabara zote za mawasiliano za nchi hiyo
May 18, 2018 03:26Sambamba na kuondoka magaidi eneo la kaskazini mwa mkoa wa Homs na kusini mwa mkoa wa Hama na kadhalika kufunguliwa barabara ya mkoa wa Homs kuelekea Damascus, mji mkuu wa Syria, jeshi la serikali limefanikiwa kudhibiti barabara zote zinazoiunganisha nchi hiyo.
-
Magaidi 19 wauawa na jeshi la Misri katika eneo la Sinai
May 17, 2018 09:29Jeshi la Misri limetangaza habari ya kuangamizwa magaidi 19 katika operesheni iliyofanywa na jeshi la nchi hiyo katika Peninsula ya Sinai.
-
Marekani inasaidia magenge stadi kuwaua wataalamu na wenye vipawa wa Kiiraqi
Apr 23, 2018 12:07Mwanachama mwandamizi wa mrengo wa Muungano wa Al-Fat'h katika uchaguzi wa Iraq amesema kuna magenge stadi ya mauaji yanayoongozwa na kuungwa mkono na Marekani ili kuwaua wataalamu na shakhsia wenye vipawa wa Kiiraqi.
-
Operesheni ya jeshi la Mali yaangamiza magaidi 15 katikati mwa nchi hiyo
Apr 22, 2018 03:25Jeshi la Mali limeeleza kupitia taarifa kuwa limewaangamiza magaidi 15 katika operesheni iliyofanywa na askari wa jeshi hilo katikati mwa nchi hiyo.
-
Magaidi elfu tano (5000) walazimika kuondoka katika viunga vya mji mkuu wa Syria
Apr 18, 2018 22:33Hatimaye, genge la kigaidi la Jeish al Islam limetangaza kuwa limekubali kuondoa wanamgambo wake 5,000 waliko katika eneo la al Dhamir katika viunga vya mji mkuu wa Syria Damascus na kuwapelekea Jarabulus mkoani Halab (Aleppo) pamoja na familia zao.