Marekani inasaidia magenge stadi kuwaua wataalamu na wenye vipawa wa Kiiraqi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i43542-marekani_inasaidia_magenge_stadi_kuwaua_wataalamu_na_wenye_vipawa_wa_kiiraqi
Mwanachama mwandamizi wa mrengo wa Muungano wa Al-Fat'h katika uchaguzi wa Iraq amesema kuna magenge stadi ya mauaji yanayoongozwa na kuungwa mkono na Marekani ili kuwaua wataalamu na shakhsia wenye vipawa wa Kiiraqi.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Apr 23, 2018 12:07 UTC
  • Marekani inasaidia magenge stadi kuwaua wataalamu na wenye vipawa wa Kiiraqi

Mwanachama mwandamizi wa mrengo wa Muungano wa Al-Fat'h katika uchaguzi wa Iraq amesema kuna magenge stadi ya mauaji yanayoongozwa na kuungwa mkono na Marekani ili kuwaua wataalamu na shakhsia wenye vipawa wa Kiiraqi.

Majidah Abdul Ilah ameliambia shirika la habari la Al-Maalumah kwamba kwa kuongoza na kuyasaidia magenge stadi ya mauaji, Marekani hadi sasa imeshaua idadi kadhaa ya wanasayansi na wataalamu wenye vipawa wa Kiiraqi na kuwafanya wengine wengi walazimike kuihama nchi baada ya kuandamwa na vitisho.

Abdul Ilah ameongeza kuwa magenge hayo yanataka kuidumaza Iraq ibaki nyuma kimaendeleo ili iendelee kuhitajia misaada ya nchi ajinabi, hasa Marekani.

Wanajeshi wa Marekani walioko nchini Iraq

Wakati huohuo gazeti la Al-Qus Al-Arabi limeandika kuwa, Abul Hassan Al-Muhajir, msemaji wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS) amesambaza mkanda wa sauti akitishia kwamba kundi hilo litavuruga uchaguzi wa bunge la Iraq unaotazamiwa kufanyika mwezi ujao wa Mei kwa kushambulia vituo vya kupigia kura.

Uchaguzi wa bunge la Iraq utafanyika tarehe 12 Mei.

Katika upande mwingine duru moja ya kiintelijinsia ya Iraq imetangaza kuwa kiongozi nambari mbili wa kundi la kigaidi la Daesh aitwaye Abu Luqman As-Suri ameangamizwa katika shambulio la anga lililofanywa hivi karibuni na jeshi la Iraq kwa uratibu na jeshi la Syria dhidi ya ngome za Daesh ndani ya ardhi ya nchi hiyo. Kiongozi huyo wa Daesh alikuwa akiongoza uandaaji magaidi na kuwapeleka Iraq kwa ajili ya kutekeleza mashambulio ya kujitoa mhanga.../