Operesheni ya jeshi la Mali yaangamiza magaidi 15 katikati mwa nchi hiyo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i43488-operesheni_ya_jeshi_la_mali_yaangamiza_magaidi_15_katikati_mwa_nchi_hiyo
Jeshi la Mali limeeleza kupitia taarifa kuwa limewaangamiza magaidi 15 katika operesheni iliyofanywa na askari wa jeshi hilo katikati mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 22, 2018 03:25 UTC
  • Operesheni ya jeshi la Mali yaangamiza magaidi 15 katikati mwa nchi hiyo

Jeshi la Mali limeeleza kupitia taarifa kuwa limewaangamiza magaidi 15 katika operesheni iliyofanywa na askari wa jeshi hilo katikati mwa nchi hiyo.

Taarifa ya jeshi la Mali imebainisha kuwa askari mmoja pia ameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa katika operesheni hiyo.

Katika miezi ya karibuni maeneo ya kati nchini Mali yamekuwa yakishuhudia mapigano makali ya umwagaji damu. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulioko nchini humo umesema una wasiwasi kutokana na jinsi hali ya usalama inavyozidi kuwa mbaya nchini Mali.

Askari wa kulinda amani wa kikosi cha MINUSMA wakiwa katika doria 

Mapinduzi ya kijeshi yalitokea nchini Mali mwaka 2012 na kufuatiwa na kuvurugika usalama wa ndani na kupata nguvu makundi ya kigaidi katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini Mali MINUSMA pamoja na wanajeshi wa Ufaransa wamekuwepo nchini humo tangu katikati ya mwaka 2013 lakini utendaji wao haujatoa mchango mkubwa katika kurejesha amani na uthabiti na kusababisha vitisho vya jinamizi la ugaidi viendelee kuiandama nchi hiyo.../