-
Hamas yapasisha pendekezo la Qatar na Misri la kuhitimisha vita vya Israel dhidi ya Gaza
Aug 19, 2025 08:06Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imesema kuwa imepasisha pendekezo jipya la Qatar na Misri la kuhitimisha vita vya mauaji ya kimbari vya Israel katika Ukanda wa Gaza
-
Hamas: Israel imeingia katika marhala mpya ya mauaji ya kimbari Gaza
Aug 17, 2025 23:57Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani vikali mpango wa Israel wa kukalia kwa mabavu Jiji la Gaza na kuwahamisha kwa nguvu wakazi wake na kusisitiza kuwa, huo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
-
HAMAS: Mpango wa Netanyahu wa 'Israel Kubwa Zaidi' ni tishio la wazi kwa mataifa ya Kiarabu na Waislamu
Aug 15, 2025 04:00Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS ametahadharisha kuhusu kupanuliwa kwa mipango ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kueleza kwamba hatua hiyo inakwenda sambamba na matamshi na ndoto za Benjamin Netanyahu kuhusu kuasisi "Israel Kubwa Zaidi."
-
Netanyahu na genge lake wapitisha mpango wa kuikalia Ghaza City, Hamas yatoa mjibizo mkali
Aug 08, 2025 07:55Liitwalo 'baraza la mawaziri la kisiasa na kiusalama' la utawala haramu wa kizayuni wa Israel limeidhinisha mpango wa waziri mkuu wa utawala huo ghasibu Benjamin Netanyahu wa kulikalia kwa mabavu eneo lote la Ukanda wa Ghaza kwa kuwahamisha kwanza kwa nguvu makumi ya maelfu ya Wapalestina wa Ghaza City.
-
HAMAS yakabidhi mapendekezo yake kuhusu makubaliano ya kusitisha vita Ghaza
Jul 24, 2025 03:22Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema katika taarifa iliyotoa mapema leo kwamba "imewasilisha majibu yake na yale ya makundi ya Wapalestina" kwa wapatanishi baada ya majuma kadhaa ya mazungumzo ya kusitisha mapigano yaliyoshindwa kuzaa matunda.
-
Marekani yajitoa tena katika UNESCO kwa sababu ya Palestina
Jul 23, 2025 03:51Marekani imeamua kujiondoa katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa mara ya pili kwa sababu ya uamuzi uliochukuliwa na shirika hilo la UN wa kuikubali Palestina kuwa nchi mwanachama.
-
Hamas yataka kukomeshwa sera ya Israel ya kuwaua Wapalestina kwa njaa
Jul 22, 2025 01:38Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imekaribisha taarifa ya pamoja ya Uingereza na nchi nyingine 24, zikitaka kusitishwa mara moja vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Gaza na kuingizwa haraka misaada ya kibinadamu katika ukanda huo uliozongirwa.
-
Hamas: Askari zaidi wa Israel watauawa iwapo mauaji ya kimbari yataendelea Gaza
Jul 19, 2025 10:06Msemaji wa Kijeshi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, ameionya Israel kuwa itapoteza wanajeshi zaidi iwapo vita dhidi ya Gaza vitaendelea.
-
Hamas: 'Jinamizi' la shahidi Deif linaendelea kuwaandama wahalifu wa kivita wa Israel
Jul 14, 2025 09:38Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imesema urithi wa kamanda aliyeuawa shahidi Mohammad Deif utaendelea kuwaandama wahalifu wa kivita wa Israel kama "ndoto mbaya".
-
Al-Qassam yamwangamiza askari wa Kizayuni baada ya kutofanikiwa kumkamata mateka
Jul 10, 2025 09:40Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS limetangaza kuwa limelazimika kumuangamiza mwanajeshi mmoja wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Ghaza baada ya mazingira kwenye medani ya mapambano kutoruhusu kumkamata mateka.