-
Iran yauandikia barua muhimu Umoja wa Mataifa na kutoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Oct 02, 2024 05:37Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua Katibu Mkuu na Rais wa Baraza la Usalama la umoja huo kufuatia operesheni ya makombora iliyofanywa na Iran, na kusisitiza kuwa, endapo utawala wa Israel utarudia tena vitendo vyake vinavyokiuka sheria za kimataifa, jibu litakalotolewa tena na Iran litakuwa la haraka, madhubiti na kali zaidi kuliko lililiotangulia.
-
Makundi ya Muqawama yaishukuru na kuipongeza Iran kwa kutekeleza Operesheni Ahadi ya Kweli 2
Oct 02, 2024 05:36Makundi ya Muqawama yamepongeza jibu kali lililotolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa utawala wa Kizayuni kufuatia Operesheni Ahadi ya Kweli 2 na kutekelezwa kwa mafanikio shambulio la makombora la Iran katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kulenga shabaha zilizokusudiwa kwa asilimia 90 ya makombora yaliyorushwa na vikosi vya ulinzi vya Iran.
-
Araghchi: Shambulio la Iran dhidi ya utawala wa Israel limetokana na haki ya uhalali wa kujilinda
Oct 02, 2024 04:39Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelitaja shambulio kali la makombora la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala katili wa Israel kuwa limeendana na haki ya halali wa kujilinda ya Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UN).
-
Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran: Bendera ya Hizbullah na Muqawama haitaanguka chini
Oct 01, 2024 10:27Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesisitiza kuwa bendera ya Hizbullah na Muqawama kamwe haitoanguka chini na amesisitiza kuwa, utawala ghasibu wa Kizayuni na Marekani watenda jinai wafahamu kwamba, hivi sasa Iran itaunga mkono zaidi kambi ya Muqawama kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
-
Rais wa Iran akosoa undumakuwili wa Marekani na Ulaya kuhusu haki za binadamu
Sep 30, 2024 22:49Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa undumakuwili wa Marekani na madola ya Ulaya kuuhusiana na haki za binadamuu na kusema, kimya cha nchi za magharibi mbele ya mauaji ya maelfu ya watu wasio na hatia ni kugonga muhuri wa kuunga mkono jinai hizi.
-
Subirini; jibu la kamanda wa jeshi la Iran kuhusu radiamali ya Tehran kwa mauaji ya shahidi Nasrullah
Sep 30, 2024 07:49Kamanda mkuu wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuhusu radiamali ya Iran na mhimili wa muqawama kwa mauaji ya Sayyid Hassan Nasrullah kuwa, subirini.
-
Iran: Marekani inataka kushadidisha taharuki katika eneo
Sep 26, 2024 00:29Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Marekani pamoja na Israel zinafuatilia kuyumbisha uthabiti na usalama wa eneo la Magharibi mwa Asia, na kupanua mvutano na mgogoro katika eneo hili.
-
Tuhuma na misimamo ya kurudiwarudiwa ya Marekani kwa ulimi wa Joe Biden katika Umoja wa Mataifa
Sep 26, 2024 00:28Jumanne ya wiki hii, rais wa Marekani, Joe Biden, alitoa hotuba yake ya mwisho katika kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York na kukariri madai ya uongo ya siku zote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na dhidi ya kambi ya Muqawama. Rais wa Marekani alidai kuwa eti serikali yake inapigania kuleta amani na utulivu katika ukanda wa Asia Magharibi.
-
Rais wa Iran: Amani inapasa kuchukua nafasi ya vita duniani
Sep 23, 2024 23:58Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, amani na usalama vinapaswa kuchukua nafasi ya vita na umwagaji damu duniani. Rais Masoud Pezeshkian amesema hayo alipoona na wakurugenzi waandamizi wa vyombo vya habari vya Marekani mjini New York na kubainisha kwamba, Iran sio kama vyombo vya habari vya dunia vinavyoinyesha na tuko tayari kuishi kwa amani na usalama na dunia nzima.
-
Akthari ya wananchi wa Marekani wanataka nchi yao irejee katika mapatano ya JCPOA
Sep 23, 2024 22:49Watu wengi nchini Marekani wanataka Washington irudi katika Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA). Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanyika huko Marekani.