Iran: Marekani inataka kushadidisha taharuki katika eneo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i116772-iran_marekani_inataka_kushadidisha_taharuki_katika_eneo
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Marekani pamoja na Israel zinafuatilia kuyumbisha uthabiti na usalama wa eneo la Magharibi mwa Asia, na kupanua mvutano na mgogoro katika eneo hili.
(last modified 2024-09-26T00:29:05+00:00 )
Sep 26, 2024 00:29 UTC
  • Iran: Marekani inataka kushadidisha taharuki katika eneo

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Marekani pamoja na Israel zinafuatilia kuyumbisha uthabiti na usalama wa eneo la Magharibi mwa Asia, na kupanua mvutano na mgogoro katika eneo hili.

Nasser Kan'ani ameashiria jinai mpya ya Wazayuni nchini Lebanon na kueleza kuwa: Utawala wa Kizayuni uliwategea vilipuzi wajumbe ambao walitumika kwa huduma na mawasiliano; uvamizi wao huo ni kitendo cha kigaidi kilichopangwa dhidi ya mauaji ya raia wa Lebanon, na kitendo kama hicho bila shaka kinaweza kufunguliwa mashtaka ya jinai (katika mahakama za) kimataifa.

Kanaani ameeleza bayana kuwa: Uongozi wa Marekani umeonyesha kwa mara nyingine tena kwamba unasimama nyuma ya jinai zote za utawala wa Kizayuni dhidi ya mataifa ya Palestina na Lebanon.

Amebainisha kuwa, utawala wa Marekani kinyume na nara zake za hadaa kuhusu haki za binadamu na maslahi yake katika kudumisha amani na usalama katika eneo, pamoja na utawala wa Kizayuni, zinalenga kuzusha hali ya wasiwasi katika eneo hili, na kuvuruga uthabiti na usalama wake.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu daima imekuwa ikionyesha kivitendo kwamba, imekuwa moja ya nguzo za kusimamisha na kuimarisha amani, utulivu na usalama katika eneo, lakini imekuwa ikichukua hatua madhubuti na ndani ya fremu ya sheria za kimataifa mkabala wa wavamizi, wachochezi, mabeberu na wavunja sheria.