Rais wa Iran: Amani inapasa kuchukua nafasi ya vita duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i116706-rais_wa_iran_amani_inapasa_kuchukua_nafasi_ya_vita_duniani
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, amani na usalama vinapaswa kuchukua nafasi ya vita na umwagaji damu duniani. Rais Masoud Pezeshkian amesema hayo  alipoona na wakurugenzi waandamizi wa vyombo vya habari vya Marekani mjini New York na kubainisha kwamba, Iran sio kama vyombo vya habari vya dunia vinavyoinyesha na tuko tayari kuishi kwa amani na usalama na dunia nzima.
(last modified 2024-09-23T23:58:28+00:00 )
Sep 23, 2024 23:58 UTC
  • Rais wa Iran: Amani inapasa kuchukua nafasi ya vita duniani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, amani na usalama vinapaswa kuchukua nafasi ya vita na umwagaji damu duniani. Rais Masoud Pezeshkian amesema hayo  alipoona na wakurugenzi waandamizi wa vyombo vya habari vya Marekani mjini New York na kubainisha kwamba, Iran sio kama vyombo vya habari vya dunia vinavyoinyesha na tuko tayari kuishi kwa amani na usalama na dunia nzima.

Daktari Pezeshkian amesema, tuna uhusiano mzuri na sawa na ulimwengu na tunaamini kwamba amani na usalama ulimwenguni unapaswa kuchukua nafasi ya vita na umwagaji damu na kwamba watu hawapaswi kuuana.

Aidha amesema, kipaumbele cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uhusiano wa kimataifa ni majirani kuelewana kwa kudumisha mipaka na usalama na kuzuia hatua zozote zinazodhuru usalama wa ndani wa kila mmoja wetu.

Akikosoa taswira ya uongo ya Iran inayoonyeshwa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za magharibi, Rais Pezeshkian amesema, nchi na taifa letu lina ustaarabu na utamaduni mkongwe na tajiri, na taswira inayotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu nchi yetu si sahihi.

Katika upande mwingine, Rais Pezeshkian amesema kuuwa, mauaji ya shahidi Ismail Haniyeh kwa hakika hayatapita bila jibu.

Vilevile amesema: Iran imethibitisha kwamba kamwe haitasalimu amri mbele ya mashinikizo na vikwazo na akaongeza: Tunatazamia maingiliano yenye kujenga, salama na yenye usawa na nchi zote za dunia.

Rais Masoud Pezeshkian siku ya Jumapili aliondoka hapa Tehran na kuelekea New York Marekani akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa kisiasa wa nchi hii kwa lengo kushiriki katika Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA.)