-
Utawala wa Kizayuni washambulia jengo la ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria
Apr 01, 2024 23:23Utawala ghasibu wa Kizayuni umetekeleza shambulio la anga dhidi ya jengo la ubalozi mdogo wa Iran karibu na ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Damascus Syria.
-
Iran: Uchunguzi wa kimataifa ufanyike kuhusu jinai ilizofanya Israel katika Hospitali ya Al-Shifa
Apr 01, 2024 23:19Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitizia ulazima wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa kuhusiana na uharibifu, utesaji na mauaji yaliyofanywa na jeshi la Kizayuni katika Hospitali ya Al-Shifa huko Ukanda wa Ghaza.
-
Ayatullah Khatami: Siku ya Quds itakuwa tofauti kabisa mwaka huu
Mar 29, 2024 08:42Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa hapa Tehran hii leo ameashiria jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kusema kuwa, hadithi ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu, itakuwa hadithi tofauti kabisa kutokana na hamasa na wingi wa watu watakaoshiriki matembezi ya siku hiyo.
-
Iran: Walimwengu wana wajibu wa kuubebesha dhima utawala wa Kizayuni
Mar 28, 2024 23:09Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameitaka jamii ya kimataifa ichukue hatua na kuubebesha dhima utawala wa Kizayuni, baada ya Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Palestina kufanya tathmini ambayo imezitaja jinai za utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza kuwa ni mauaji ya kimbari.
-
Iran yazitaka IPU, NAM kufanya juhudi za kusitisha vita Gaza
Mar 27, 2024 04:11Iran imetoa mwito kwa Jumuiya ya Kimataifa ya Mabunge (IPU) na Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) kuchukua hatua za maana na za kivitendo kusitisha mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akosoa undumakuwili wa Magharibi
Mar 26, 2024 04:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumza kwa simu na mwakilishi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya katika Masuala ya Nje na Sera ya Usalama na kukosoa vikali vigezo vya undumakuwili na vinavyokinzana vya nchi za Magharibi mkabala wa Palestina na Gaza.
-
Mkutano wa Umoja wa Mabunge unaendelea Geneva kwa kuhudhuriwa na Iran
Mar 25, 2024 08:31Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani, kama chombo kikubwa zaidi cha utungaji sheria chenye nchi wanachama zaidi ya 180, ukiwemo ujumbe kutoka Iran unafanyika mjini Geneva Uswisi kwa kauli mbiu ya "Diplomasia ya Bunge, Ujenzi wa Daraja la Amani na Maelewano".
-
Shirikisho la Soka la Iran likaribisha pendekezo la Wapalestina la kuwekewa vikwazo Shirikisho la soka la Israel
Mar 25, 2024 08:14Mkuu wa Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia barua Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), akikaribisha mpango uliopendekezwa wa Shirikisho la Soka la Palestina kuhusu kuwekewa vikwazo Shirikisho la Soka la utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Iran na Oman zasisitizia udharura wa kukomeshwa mara moja jinai za Israel Ghaza
Mar 25, 2024 02:43Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman wamefanya mazungumzo ya simu na kutilia mkazo wajibu wa kuchukuliwa hatua za haraka na jamii ya kimataifa za kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhlumu na wasio na ulinzi wa Palestina hasa wa Ukanda wa Ghaza.
-
Wairani waandamana kulaani jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza
Mar 24, 2024 23:21Wananchi wa Iran wamefanya maandamano makubwa katika sehemu mbalimbali za nchi ukiwemo mji mkuu Tehran, kutangaza mshikamano na wananchi madhulumu wa Palestina wanaoendelea kuuawa, sambamba na kulaani jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.