-
Pezeshkian: Iran, Saudia zinaweza kuwa kielelezo cha ushirikiano wa kikanda
Apr 18, 2025 07:16Rais wa Iran Masoud Pezeshkian wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu na Saudi Arabia zinaweza kuwa kielelezo cha ushirikiano wa kieneo na kusisitiza kuwa, umoja wa nchi za Kiislamu ni sharti la kupatikana amani, usalama na maendeleo endelevu ya kiuchumi katika eneo hili.
-
Waziri wa Ulinzi wa Saudia yupo Tehran kujadili uhusiano wa pande mbili, masuala ya kieneo
Apr 17, 2025 13:35Waziri wa Ulinzi wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Khalid bin Salman Aal-Saud amewasili Tehran leo Alkhamisi kwa ziara muhimu inayolenga kuimarisha uhusiano wa pande mbili wa Tehran na Riyadh, na kujadili masuala ya kieneo.
-
Araghchi: IAEA inaweza kutatua kwa amani faili la nyuklia la Iran
Apr 17, 2025 12:59Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesema Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) unaweza kuwa na nafasi na jukumu muhimu katika utatuzi wa amani wa suala la nyuklia la Jamhuri ya Kiislamu.
-
Grossi asisitiza nafasi ya diplomasia katika suala la nyuklia la Iran
Apr 17, 2025 12:43Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), aliwasili Tehran Jumatano, Aprili 16, ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Sayyid Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, na Mohammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran.
-
NYT: Trump alipinga pendekezo la Israel la kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran
Apr 17, 2025 12:41Rais wa Marekani, Donald Trump amekataa pendekezo la Israel la kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran, gazeti la New York Times liliripoti hayo Jumatano jioni, likiwanukuu maafisa wa Ikulu ya White House na maafisa wengine wanaofahamu suala hilo.
-
Iran yasisitiza kuhusu kulindwa misingi ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa
Apr 16, 2025 02:19Katika mkutano wa ngazi ya juu wa Kundi la Marafiki wa Kulinda Mkataba wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Moscow, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisheria na kimataifa, Kazem Gharibabadi, amesisitiza umuhimu wa kufufua mfumo wa kimataifa wa pande nyingi (multilateralism) na kulinda misingi ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
-
Kuimarishwa biashara kati ya Iran na Eurasia; hatua ya kimkakati
Apr 15, 2025 14:44Biashara kati ya Iran na Umoja wa Kiuchumi wa Nchi za Eurasia imekuwa ikistawi siku hadi siku licha ya vikwazo vikubwa vya kiuchumi vilivyowekwa na Magharibi dhidi ya Iran. Kwa mujibu wa tawimu mpya zilizotolewa hivi karibuni, uuzaji bidhaa za Iran kwa nchi wanachama wa umoja huo katika mwaka uliopita uliongezeka kwa asilimia 20 na kufikia karibu dola bilioni mbili.
-
Iran yabainisha wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya watu wa Al-Fasher, Sudan
Apr 15, 2025 10:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amebainisha wasiwasi wake juu ya hali mbaya ya kibinadamu ya watu wa mji wa Al-Fasher uliozingirwa huko Sudan, na ametaka kuondolewa kwa mzingiro huo, kusitishwa kwa mashambulizi, na kulindwa kwa maisha ya raia kwa mujibu wa misingi ya sheria za kimataifa za kibinadamu.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudia wajadili mazungumzo ya Oman
Apr 15, 2025 08:06Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudi Arabia wamefanya mazungumzo ya simu na kujadiliana kuhusu uhusiano wa pande mbili na maendeleo ya kikanda na kimataifa.
-
Wanachuo wa Iran waendeleza maandamano ya kuiunga mkono Palestina
Apr 15, 2025 07:23Wanafunzi, maprofesa, wahadhiri na wafanyakazi wa Vyuo Vikuu vya mikoa ya Ardabil na Khorasan Kusini wamefanya maandamano ya kulaani ghasia na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza.