-
EU: Mazungumzo ya Vienna yamefika katika marhala hasasi
Feb 22, 2022 23:10Naibu Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema mazungumzo ya Vienna yenye lengo la kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yanaelekea ukingoni, na hivi sasa yako katika marhala hasasi na nyeti.
-
Rais Ebrahim Raisi: Gesi asilia itaunda mustakbali wa nishati duniani
Feb 22, 2022 09:31Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika Mkutano wa Jumuiya ya Nchi Zinazouza Nje Gesi Asilia (GECF) kwamba gesi asilia inaunda mustakbali wa nishati ya dunia na ni chanzo muhimu cha nishati kwa ajili ya jamii.
-
Safari ya Raisi nchini Qatar, maonyesho ya diplomasia ya ujirani mwema
Feb 21, 2022 06:29Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema leo amewasili Doha mji mkuu wa Qatar kwa mwaliko wa Amir wa nchi hiyo, kuhudhuria Mkutano wa Sita wa Jumuiya ya Nchi Zinazouza Nje Gesi Asilia (OPEC-Gas) sambamba na kuimarisha uhusiano wa pande mbili.
-
Amir Abdollahian afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Lebanon, Katibu Mkuu wa UN na wawakilishi wa nchi mbalimbali mjini Munich
Feb 20, 2022 09:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Lebanon pambizoni mwa Mkutano wa 58 wa Usalama wa Munich.
-
Mazungumzo ya Marais wa Iran na Ufaransa sanjari na hatua muhimu za mazungumzo ya Vienna
Feb 20, 2022 08:49Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo yake ya simu na Rais wa Ufaransa kwamba suala kuu litakalosaidia kufikiwa mapatano mjini Vienna ni kuhakikisha maslahi ya wananchi wa Iran yanalindwa hususan kuondolewa vikwazo, kupewa dhamana madhubuti na kufungwa mafaili ya madai ya kisiasa.
-
Iran yaitaka dunia ikomeshe jinai za Israel dhidi ya Wapalestina
Feb 20, 2022 04:33Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka za kuuzuia utawala wa Kizayuni wa Israel kuendelea kufanya jinai na uhalifu dhidi ya Wapalestina.
-
Raisi: Makubaliano yoyote ya Vienna sharti yajumuishe kuondolewa vikwazo Iran
Feb 20, 2022 00:18Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mapatano yoyote yatakayofikiwa kwenye mazungumzo ya Vienna yenye lengo la kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA lazima yajumuishe suala la kuondolewa vikwazo taifa la Iran, sanjari na kupasishwa kwa kipengee kuhusu dhamana yenye itibari, na vile vile kujizuia na masuala ya kisiasa na kuibua tuhuma zisizo na msingi.
-
Iran yafanyia majaribio yaliyofana chanjo ya kukabiliana na Omicron
Feb 16, 2022 23:49Shirika la Kutengeneza Dawa la Shifa la Iran limetangaza mafanikio makubwa ya awali katika majaribio ya chanjo ya kukabiliana na COVID-19 aina ya Omicron.
-
Iran: Tuko tayari kushiriki katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa
Feb 16, 2022 03:42Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kushiriki katika operesheni za kulinda amani za umoja huo katika maeneo mbalimbali duniani.
-
Shamkhani: Mienendo hasi ya US ndilo tishio kuu kwa mapatano yoyote yale
Feb 15, 2022 23:17Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema siri ya kufikiwa mapatano mazuri kwenye mazungumzo ya kuiondolea vikwazo haramu Jamhuri ya Kiislamu ni Tehran kupewa dhamana ya kisheria ambayo itaifanya Marekani isiweze kujitoa kwa mara nyingine tena ndani ya mapatano ya JCPOA.