-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Jamhuri ya Kiislamu inatokana na mapinduzi makubwa ya Kiislamu
Mar 29, 2019 11:38Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatokana na mapinduzi makubwa ya Kiislamu."
-
Iran yatahadharisha: Israel inaunda muungano na magaidi
Mar 29, 2019 11:31Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetahadharisha kuwa, utawala ghasibu wa Israel, ambao unatoa uungaji mkono kwa magaidi nchini Syria, unaweza kuunda muungano na magaidi hao iwapo tishio lao halitashughulikiwa ipasavyo.
-
Igizo jengine la Pompeo la uenezaji hofu na chuki dhidi ya Iran
Mar 29, 2019 00:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo ameifufua tena kampeni ya uenezaji hofu na chuki dhidi ya Iran kwa kuituhumu Jamhuri ya Kiislamu kwa kile alichodai, nafasi haribifu iliyonayo katika eneo la Magharibi ya Asia na kuunga mkono ugaidi.
-
Qassemi: Marekani ifahamu haiwezi kupora utajiri wa Iran
Mar 28, 2019 03:31Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria hukumu ya Mahakama ya Luxembourg ambayo imekataa ombi la Marekani la kuchukua udhibiti wa mali za Benki Kuu ya Iran na kusema: "Marekani inapaswa kufahamu kuwa, kwa kutumia hadaa haiwezi kupora utajiri na milki za Wairani.
-
"Chuki dhidi ya Iran" (Iranophobia) ni sera ya pamoja ya Marekani na Utawala wa Kizayuni
Mar 25, 2019 07:57Jitihada za kushadidisha "Chuki dhidi ya Iran" (Iranophobia) ni ajenda daima ya sera za pamoja na utawala wa Kizayuni wa Israel. Maudhui hii ni moja kati ya ajenda muhimu ambazo Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu, anafuatilia katika safari yake nchini Marekani.
-
Majeshi ya Iran yanawafikishia misaada waathirika wa mafuriko kaskazini mwa nchi
Mar 24, 2019 11:13Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Meja Jenerali Mohammad Baqeri amesema kuwa, vikosi vya ulinzi humu nchini vinaendesha oparesheni kamili ya kuwasaidia waathirika wa mafuruko kaskazini mwa nchi.
-
Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran; na bwabwaja za Mike Pompeo
Mar 23, 2019 21:56Kutekeleza siasa za kuyawekea vikwazo mataifa mengine hususan wapinzani na mahasimu wa Marekani, ni moja ya nguzo kuu za siasa za kigeni za Washington katika duru ya uongozi ya Rais Donald Trump.
-
Kukariri Trump porojo lake katika ujumbe wa Nowruz kwa Wairani
Mar 22, 2019 03:12Rais wa Marekani Donald Trump, tangu kwenye kampeni zake za uchaguzi wa rais na mpaka baada ya kuingia Ikulu ya White House Januari 2017, amekuwa akitumia lugha kali na maneno machafu dhidi ya Iran, kwa lengo la kuudhoofisha na kuuangusha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Rais Rouhani katika ujumbe wa Nowruz mwaka 1398: Taifa la Iran kwa yakini litapata ushindi
Mar 21, 2019 00:23Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema Alhamisi ametuma ujumbe kwa kunasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1398 Hijria Shamsiya na kusema mwaka 1397 ulikuwa mwaka wa mafanikio makubwa ya taifa la Iran katika nyuga mbali mbali na kuongeza kuwa, kwa yakini taifa la Iran litapata ushindi na litavuka matatizo yaliyopo.
-
Mazungumzo ya kisiasa ya Brussels na Tehran; kukiri Umoja wa Ulaya juu ya nafasi muhimu ya kieneo ya Iran
Mar 20, 2019 10:37Licha ya njama mtawalia za serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani za kudhoofisha nafasi muhimu ya kieneo ya Iran kwa kueneza sera za chuki dhidi ya taifa hili, lakini pamoja na hayo yote madola makubwa ya dunia yamekuwa yakisisitiza juu ya nafasi muhimu na isiyokanushika ya Tehran katika Mashariki ya Kati na kukiri dhahir shahir kuhusiana na jambo hilo.