-
Russia na China zasimama na Iran dhidi ya E3 kwa kutumia vibaya azimio la UN
Aug 29, 2025 04:08Russia na China zimechukua hatua kukabiliana na mpango wa nchi tatu zinazounda Troika ya Ulaya, E3, na kusambaza rasimu ya azimio katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalopendekeza "urefushaji wa kiufundi" kwa muda wa miezi sita utekelezaji wa Azimio 2231 la baraza hilo.
-
Rais Pezeshkian asisitizia haja ya kuimarisha uhusiano wa Iran na Madagascar
Aug 28, 2025 23:46Rais Masoud Pezeshkian amewataka mabalozi wapya walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu katika nchi za Madagascar na Croatia kuimarisha uhusiano wa pande mbili baina ya Iran na nchi hizi mbili.
-
Iran yalaani vikali hatua ya E3 kutekeleza "snapback", yasema haina uhalali kisheria
Aug 28, 2025 23:46Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali uamuzi uliochukuliwa na Ufaransa, Ujerumani na Uingereza siku ya Alkhamisi wa kuanzisha utaratibu wa "snapback" wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kurejesha papo kwa papo vikwazo vya baraza hilo dhidi yake kutokana na mpango wake wa nyuklia.
-
Aliyeua watoto kwa bunduki katika skuli ya kanisa Marekani ni mwanamume aliyebadilisha jinsia
Aug 28, 2025 02:36Mshambuliaji aliyefyatulia risasi kanisa katika skuli ya kikatoliki kusini mwa mji wa Minneapolis nchini Marekani jana Jumatano na kuua na kujeruhi watu kadhaa ametambuliwa na gazeti la The New York Post kama Robin Westman. Kwa mujibu wa gazeti hilo, inasemekana Westman alibadilisha jina lake la Robert na kuwa Robin mwaka 2020 na kujitambulisha kama mwanamke.
-
Polisi ya Iran yaangamiza magaidi 8 waliohusika na shambulizi la kigaidi Sistan na Baluchestan
Aug 27, 2025 07:16Polisi ya Iran imetoa kipigo kikubwa kwa magaidi wanaoungwa mkono na nchi ajinabi katika mkoa wa Sistan na Baluchestan, kusini-mashariki mwa Iran, kwa kuwaangamiza magaidi 8 waliohusika na shambulio baya la karibuni dhidi ya maafisa wa polisi katika mkoa huo.
-
Pezeshkian amwambia Putin: Iran haijawahi kamwe kutaka kumiliki silaha za nyuklia
Aug 26, 2025 00:12Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Jumatatu alizungumza kwa simu na Rais Vladimir Putin wa Russiai na kumweleza kuwa Tehran haijawahi kutaka kumiliki wala haitatafuta silaha za nyuklia, akisisitiza msimamo wa muda mrefu wa Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia.
-
Araghchi: Historia haitasamehe usuasuaji zaidi katika kukomesha janga la Gaza
Aug 25, 2025 08:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi ametoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti za kimataifa kukomesha mauaji ya halaiki ya Israel yanayoendelea huko Gaza, akisema kuwa nchi zote zinapaswa kusimama upande sahihi wa historia ambao "hautasamehe" ucheleweshaji wowote zaidi wa kupunguza mateso ya watu wa Palestina.
-
Pezeshkian: Migawanyiko kati ya mataifa ya Kiislamu inainufaisha Israel pekee
Aug 25, 2025 07:30Rais wa Iran amesema umoja wa wananchi wa Iran na katika mataifa yote ya Kiislamu ndiyo kinga kuu dhidi ya vitisho vya maadui, akionya kuwa migawanyiko ni kwa maslahi ya Israel pekee.
-
Iran na Ulaya kuendelea na mazungumzo ya nyuklia mjini Geneva
Aug 25, 2025 07:03Iran na nchi tatu zenye nguvu za Ulaya - Ujerumani, Ufaransa na Uingereza - zinatazamiwa kuanza tena mazungumzo ya nyuklia huko Geneva, Uswisi siku ya Jumanne, yakiangazia maswala ya nyuklia na uondoaji wa vikwazo.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran itasimama kidete dhidi ya matakwa ya Marekani
Aug 24, 2025 09:35Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema Marekani inahujumu na kukabiliana na Iran kwa sababu inataka taifa hili liwe tiifu kwake, lakini wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu watapambana vikali na “tusi hilo kubwa”.